Latest Posts

RC MALIMA AMTAKA DC MPYA MVOMERO KUZINGATIA KIAPO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amemtaka Mkuu mpya wa Wilaya ya Mvomero, Maulid Hassan Dotto, kuchukua majukumu yake kwa umakini na kuzingatia viapo alivyoviapa, hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Malima amesema hayo leo Juni 27, 2025 mkoani Morogoro wakati wa hafla ya kumuapisha Dotto ambapo amesisitiza kuwa nafasi ya ukuu wa Wilaya ni ya heshima kubwa, inayohitaji uadilifu, maarifa, ushirikiano, pamoja na utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

kwa upande wake, Selemani Shabani Selemani Kaimu Katibu Msaidizi Kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Kanda ya Mashariki amemshauri Mkuu huyo mpya wa Wilaya kuendelea kujifunza katika utendaji wake wa kazi ili aweze kutekeleza vyema majukumu ya kila siku na kulisaidia Taifa kwa ujumla.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro Nuru Ngereja ameeleza kuwa chama kina matarajio makubwa kwa uongozi wa Dotto na kuamini kuwa chini ya usimamizi wake, heshima na nguvu ya CCM katika Wilaya ya Mvomero vitaimarika, na ushirikiano kati ya chama na serikali utaendelea kuimarishwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!