Latest Posts

WAZALISHAJI WATAKIWA KUTUMIA NEMBO MPYA KWENYE BIASHARA

Wazalishaji wa bidhaa na watoa huduma nchini wametakiwa kukamilisha taratibu za utambulisho kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na kuweka nembo ya Made in Tanzania ili kulinda bidhaa na huduma zao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, wakati wa maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, ambayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kuitangaza nembo ya biashara ya Tanzania.

Amesema kuwa matumizi ya nembo hiyo yatasaidia kuzitangaza bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuwapa wazalishaji ushindani wa haki, na hatimaye kushindana kwa ubora badala ya bei.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara amesema nembo hiyo inabeba uzito wa kipekee katika sekta ya biashara nchini, kwani inaenda kuondoa changamoto ya bidhaa za Kitanzania kutotambulika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!