Theophilida Felician, Kagera.
Katibu mkuu wa chama cha waganga TAMESOT Bw. Lukas Joseph Mlipu ametoa wito akiwataka waganga wa tiba asili nchini kufanya kazi kwa umakini hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025.
Katibu huyo ameyabainisha hayo wakati akiwahutubia waganga kwenye semina iliyofanyika kata ya Kibeta manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambapo amefafanua kuwa imezoeleka nyakati kama hizi  waganga huwa kimbilio la wanasiasa kupata tiba kwa namna mbalimbali hivyo ni wajibu wao kuwa chonjo kwani  yamekuwepo mambo mengi yanayotendeka kwenye jamii mfano mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino yakishatokea huwahusisha moja kwa moja waganga jambo ambalo siyo jema.
“Tuepuke uhalifu ndugu zanguni inatokea mtu anakatakata mtu huko anakimbilia kwako eti apate dawa asikamatwe  nawewe unapambana kwelikweli kumsaidia huo sini uhalifu?”sasa ukibainika unafanya hivyo wakukamate”amesema katibu mkuu Lukas Mlipu.
Hata hivyo akiwa mkufunzi wa mafunzo  yaliyolenga kuwanoa waganga ili kuwajengea uwezo na weledi amewasisitiza kuwa TAMESOT imejipanga kuinua sekta hiyo ambayo imekuwa ikizipitia changamoto kadhaa hasahasa kudharauliwa, kubezwa, kuonewa namengineyo huku akiwasihi kuwa wamoja nakukijenga chama hicho kwa vitendo.
ACP Mpondera Rashidi ni mkuu wa polisi jamii mkoa Kagera kwaniaba ya kamanda wa polisi mkoa amewaeleza kwamba baadhi ya waganga wamekuwa wakihusishwa na ramuli chonganishi na kufanya kazi bila leseni mambo ambayo ni kinyume na taratibu
Mpondera ameongeza kuwa kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais TAMESOT haina budi kuwasimamia kikamilifu waganga wasihusishwe na matukio ya namna yoyote  kinyume na leseni zao.
Yustas Nyakubaho ni mwenyekiti wa waganga wilaya Ngara akishukuru na kupongeza juhudi za katibu Mkuu Lukas Joseph Mlipu  amewakumbushia madhira waliyoyapitia kipindi cha wimbi la mauaji ya Albino hivyo ametoa wito akiwasihi wenzake wasiingizwe mitegoni na watu wasiokuwa na nia njema na taaluma hiyo