Mashuhuda walieleza kuwa mwanamke huyo, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, alionekana akiwa na furaha awali alipokuwa akizungumza na dada yake wa tumbo, lakini ghafla alianza kumwimbia nyimbo zisizoeleweka, kabla ya kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine.
Dada yake, ambaye alionekana kushangazwa na kitendo hicho, alijaribu kumzuia lakini mwanamke huyo alimshika kwa nguvu na kumkumbatia kwa nguvu huku akiendelea kuimba na kucheka ovyo.
“Alianza kwa sauti ya kawaida, kama anaimba nyimbo za injili, lakini ghafla sauti yake ikabadilika, ikawa nzito na ya kutisha, kisha akasema kuna sauti inamwambia avue nguo,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo. Soma zaidi hapa.