Latest Posts

RAIA 39 WA BURUNDI WAKAMATWA GEITA KWA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA

Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji mkoani Geita imefanikiwa kuwakamata raia 39 kutoka Burundi waliodaiwa kuingia nchini kinyume cha taratibu za uhamiaji na kufanya shughuli za kilimo katika Pori la Nshinde, eneo nyeti lililopo mpakani mwa Halmashauri ya Manispaa ya Geita na Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Geita, Mrakibu Mwandamizi Donald Lyimo, amethibitisha kukamatwa kwa raia hao, akieleza kuwa ni sehemu ya operesheni inayoendelea katika vijiji mbalimbali mkoani humo, hatua inayolenga kulinda usalama wa mipaka na rasilimali za taifa.

Ameongeza kuwa katika msako huo pia wamewakamata Watanzania wawili kwa tuhuma za kuwapangisha makazi raia hao na kuwatumikisha katika shughuli za kilimo.

Kwa upande wao, baadhi ya raia hao wa Burundi waliokuwa katika ofisi za uhamiaji mkoani Geita wamesema wameingia Tanzania kutokana na ugumu wa maisha nchini kwao, hali iliyowalazimu kutafuta ajira ya kuwaingizia kipato.

Jeshi la Uhamiaji mkoani Geita limeahidi kuendelea na operesheni hizo kwa lengo la kudhibiti uingiaji holela wa raia wa kigeni nchini sambamba na kuhakikisha sheria za uhamiaji zinazingatiwa ili kulinda usalama na masilahi ya taifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!