Latest Posts

KAYA MTWARA ZASISITIZWA KUPANDA MITI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Mradi wa mabadiliko ya tabianchi na kupunguza atari za maafa unaotekelezwa na Mtandao wa HakiRasilimali mkoani Mtwara umeonyesha matokeo chanya katika kuhifadhi mazingira na kuongeza hamasa ya wananchi kupanda miti.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo katika kikao cha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa mabadiliko ya tabianchi na kupunguza athari za maafa Afisa wa HakiRasilimali Rajabu Mnihama amesema hatua kadhaa zimeanza kuonekana ikiwemo taasisi husika kuchukua hatua kwa wanaokata miti kinyume cha sheria, viongozi kutenga maeneo maalum ya upandaji miti na kuanzishwa kwa vitalu katika kata mbalimbali.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara, Wakili Richard Mwalingo, ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kuhifadhi na kutunza mazingira, akisisitiza kila kaya kupanda angalau miti mitano ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Washiriki wa kikao hicho wakiwemo waandishi wa habari, taasisi za serikali na asasi zisizo za kiserikali wamesema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza uelewa wa jamii kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli za binadamu.

 

Mradi huo umetekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja katika halmashauri tatu za mkoa wa Mtwara ambazo ni Manispaa ya Mtwara Mikindani, Halmashauri ya Mtwara DC na Halmashauri ya Mji Newala.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!