Latest Posts

ANAYEDAIWA KUMFANYIA UKATILI NEEMA NAIROT AKAMATWA

Mwanaume aliyetambulika kwa jina la Matunda Longido (29) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumfanyia kitendo cha ukatili wa kijinsia Neema Nairot, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, Jeshi la Polisi limechukua hatua za kisheria baada ya kupokea taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu tukio hilo, ambalo linadaiwa kumhusisha mchumba wa mwanafunzi huyo kwa kushirikiana na familia yake.

Aidha, Jeshi la Polisi limechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufanya ufuatiliaji wa kina ili kubaini ukweli wa tukio, kumkamata mtuhumiwa na kumhifadhi mwanafunzi huyo katika makazi salama kwa ajili ya ulinzi pamoja na msaada wa kisaikolojia.

Kamanda Mkama amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vingine vya haki jinai, ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote watakaobainika kuhusika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!