Latest Posts

ADC YAMTAKA KIKWETE KUOMBA RADHI KWA KAULI YA “PUMBA NA MCHELE”

Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Taifa, Shaban Itutu, amemtaka Rais mstaafu wa Tanzania na Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuomba radhi kwa umma wa Watanzania kutokana na kauli yake kuhusu ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Itutu ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akihutubia mkutano wa kampeni wa chama hicho uliofanyika Buguruni, jijini Dar es Salaam, saa chache baada ya hotuba ya Kikwete.

Kwa mujibu wa Itutu, kauli ya Kikwete kwamba “CCM hawapo tayari kuchanganya pumba na mchele” iliyotajwa kumaanisha kuwa wabunge wote wanatakiwa kuwa wa chama hicho, inaleta mashaka juu ya mustakabali wa demokrasia nchini.

“Sisi tukiwa tumejitoa kimasomaso kuionesha demokrasia ndani ya nchi yetu inatakiwa kuendelea kuwepo na kuilinda, leo Rais Mstaafu mbele ya wananchi wa Tanzania na vyombo vya habari anawaambia Watanzania kwamba CCM hawapo tayari kuchanganya pumba na mchele”, amesema Itutu.

Katika mkutano wa kampeni wa CCM mkoani Pwani, Kikwete alisema Watanzania wana kila sababu ya kumchagua mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa amefanikisha kukabili changamoto nyingi zinazowakabili wananchi, hivyo ni muda wa kulipa wema huo.

“Ninakuhakikishia kuwa wananchi wa Mkoa wa Pwani tutawachagua wabunge wote wa CCM, na ni imani yangu kuwa Tanzania nzima itakuwa hivyo. Hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele,” alisema Kikwete.

Itutu amesema angetarajia kauli za kuhamasisha ushindani wa kidemokrasia na siyo kuelekeza ushindi wa upande mmoja.

“Mimi ningetegemea angesema tunakwenda kushindana na wenzetu, atakayeshinda atangazwe, atakayeshindwa abaki asitangazwe, hizo ndizo kauli za kidemokrasia na kauli za kidemokrasia za wanademokrasia waliokomaa kama Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete”, ameeleza.

“Mimi ningetegemea angesema tunakwenda kushindana na wenzetu, atakayeshinda atangazwe, atakayeshindwa abakie, hizo ndizo kauli za kidemokrasia kutoka kwa viongozi waliokomaa,” alisema Itutu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!