Latest Posts

DIT YAZIDI KUKUBALIKA KIMATAIFA TEKNOLOJIA YA ANGA NA SATELAITI

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imezidi kuimarisha ushirikiano wake kimataifa katika teknolojia ya anga na satelaiti ikiwa ni sehemu ya mikakati yakutekeleza agizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuzindua satelaiti yake ya kwanza ifikapo Agosti 01, 2026.

Katika sehemu ya mashirikiano hayo, DIT imetembelewa na Mkuu wa Chuo Kikuu mashuhuri nchini Urusi, cha RUDN, Prof. Oleg A. Yastrebov, tarehe 07 Oktoba 2025 ambaye pamoja na mambo mengine ameipongeza DIT kwa udhubutu wake katika teknolojia ya Anga na Satelaiti na kuahidi ushirikiano katika uhamishaji wa Teknolojia (Technology Transfer) baina ya Rudn na DIT.

Aidha Prof.Yastrebov ameahidi kuendelea kusaidia DIT katika kuwajengea uwezo wafanyakazi katika nyanja za teknolojia ya anga na satelaiti.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Marco Ndomba amekishukuru Chuo Kikuu cha RUDN kwa kuunga mkono juhudi za DIT katika teknolojia ya Anga na Satelaiti kwenye kujenga uwezo kwa wafanyakazi kwa kumualika na kumsaidia mmoja wa wafanyakazi wa DIT, Dk. Petro Pesha, kushiriki katika kitengo cha kisayansi katika mkutano wa “Russia-Africa” uliofanyika St. Petersburg kuanzia tarehe 25 hadi 29 Julai 2023.

Prof. Ndomba ameeleza kuwa ushirikiano baina ya DIT na Chuo Kikuku cha RUDN imechagizwa pakubwa na ushirikiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Taifa la Tanzania na Urusi.

DIT na Rudn zilitia saini programu za ushirikiano katika elimu na utafiti mnamo tarehe 1 Desemba 2023, zikiwa na lengo la kuimarisha elimu ya pamoja na tafiti katika maeneo ya akili unde (AI) Ujifunzaji wa Mashine (ML) utafiti wa anga na matumizi yake.

Aidha Prof. Ndomba amemsihi Prof. Yastrebov kuendelea kutoa fursa ya ushirikiano katika maeneo ya kubadilishana wahadhiri, nafasi masomo kwa wanafunzi, tafiti na ubunifu, pamoja na programu za shahada za pamoja hasa katika maeneo ya Teknolojia ya Anga na Satelaiti, Akili Unde (AI), Roboti, na Mtandao wa Vitu (IoT)

“DIT itathamini mchango wako katika kuwezesha miunganisho ya kujenga uwezo wa wafanyakazi katika kutengeneza na kupima satelaiti kupitia ROSCOSMOS na taasisi nyingine za teknolojia ya anga nchini Urusi” Amesisitiza Prof. Ndomba.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!