Latest Posts

WATUMISHI WA TEA WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA NEST

Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo wamepatiwa mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi wa Kidijitali (NEST), yaliyotolewa na Mkufunzi kutoka Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Bw. Ali Shaali.

Mafunzo hayo, yaliyofanyika katika ofisi za TEA, yalilenga kuwajengea uwezo watumishi katika kutumia mfumo huo kwa ufanisi zaidi katika mchakato wa manunuzi ya umma.

Bw. Shaali alisema kuwa mfumo wa NEST ulianza kutumika mwaka 2023 na umeleta manufaa mbalimbali, ikiwemo kuharakisha michakato ya manunuzi na kudhibiti mianya ya udanganyifu.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani manunuzi ya umma ni eneo mtambuka linalohusisha watumishi kutoka sekta na idara mbalimbali ndani ya taasisi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!