Latest Posts

TAMESOT YAJA NA MIPANGO THIBITI ILI KUYAFIKIA MALENGO

 

Na Theophilida Felician.

Chama cha waganga wa tiba asili na tiba mbadala nchini TAMESOT kimeelezea mwelekeo mpya wenye malengo thabibi utakaowezesha kuongeza ufanisi na uimara wa chama katika utekelezaji wa majukumu ya kuiinua tiba asili.

Kauli hiyo imetolewa naye katibu mkuu wa chama hicho Bw Lukas Joseph Mlipu akifanya mazungumzo na chombo hiki kwa njia ya simu akiwa kwenye ziara Chato Mkoani Geita.

Katibu mkuu huyo amesema TAMESOT yenye makao makuu yake mkoani Dodoma ni chama ambacho kimejizatiti na kuwajibika kwa namna mbalimbali ya kuijenga taaluma ya tiba asili hususani kutoa elimu yenye kuakisi ubora wa tiba kwa jamii hivyo ili kuendeleza juhudi hizo chama kimeandaa dira iliyoyajumuisha mambo kadha wa kadha ili kuongeza kasi na kupiga hatua mbele kimaendeleo.

Baadhi ya vipaumbele katika dira hiyo amevitaja kuwa ni pamoja na elimu inayoyagusa maeneo tafauti tofauti hasa uzalendo, kujali muda, uongozi uliobora na wenye kufanyakazi kwa kuzingatia misingi na miongozo ya katiba ya chama, uadilifu, kujitegemea ili kuwa huru katika utekelezaji wa majukumu ya kusimamia nakujenga heshima ya taaluma hatimaye waganga kuthaminiwa nyanja zote, kuimalisha afya na uchumi wa taifa kwa ujumla sambamba na kuendeleza kitengo cha tafiti na ubunifu.

Akitoa ufafanuzi eneo la uongozi bora amesema ni eneo muhimu na nyeti hivyo taasisi itahakikisha viongozi wanaoitumikia wanafanya kazi kwa weledi kutokana na katiba kusheheni miongozo sahihi na hategemei kiongozi yeyote kwenda kinyume na maelekezo ya katiba hiyo.

Ameongeza kwamba viongozi wakifanya kazi kwakufuata katiba itasaidia kuziondoa changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa baadhi ya viongozi hususani kushindwa kutimiza wajibu ipasavyo kiutendaji.

Hata hivyo amehitimisha akiwasihi waganga kuendelea kutoa huduma ya tiba asili kulingana na miongozo ya serikali chini ya baraza la tiba asili na tiba mbadala huku akiwataka kujiepusha na mambo yanayoweza kuwaingiza katika changamoto hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!