Latest Posts

GRUMETI FUND YAWAPELEKA WANAFUNZI UGHAIBUNI KUJIFUNZA MADILIKO YA TABIANCHI

Shirika la Grumeti Fund limewapeleka wanafunzi 2 nchini Taiwan ili kujifunza namna bora ya kukabilina na mbadilikao ya Tabia nchi, pamoja nanamna bora ya upandaji miti na utunzaji wa maliasili, mazingira, vyanzo vya maji na kubadilisha taka kuwa fursa kwenye maeneo yao.

Wanafunzi hao ikiwa nikati ya wanafunzi 32 kutoka shule 16 zilizoko kwenye program ya Elimu ya Mazingira ambayo imekuwa ikifanywa na Grumeti fund ambapo wanafunzi 512 hufikiwa kila mwaka na program hiyo.

Akizungumza wakati wakutimiza adhima hiyo ya wanafunzi hao ambao wamepatikana baada ya mashindano hayo kukamilika mkuu wa kituo cha Elimu ya mazingira Grumeti fund Laurian Lamatus alisema kupitia kituo hicho nikuwafundisha wanafunzi kuhusu maliasili pamoja na uhifadhi wa mazingira.

“Katika kipindi hiki tuliendesha mdahalo ambao tulipata wanafunzi 32 bora ke 16 na wanaume 16 tulipata wanafunzi washindi wa wili kutoke isenye na Natta katika pongezi walizopata nisafari ya kwenda Taiwan walialikwa na watakaa huko kwa siku 10 na watapata fursa ya kujifunza mazingira sana nk.”Alisema Laurian Lamatus Mkuu wa kituo cha Elimu ya Mazingira EEC.

Pia Laurian alisema kila jumatano wamekuwa na mdahalo na miongoni mwa shule kutoka Taiwan ili kuwapa changamoto ya kubaini madiliko ya Tabia nchi kutoka kwenye taifa hilo kulingana na wao wanaishi katika maeneo ya mapori ya akiba hii tunawatengenezea kulinda mazingira.

Kwa uapnde wa Frida Mollel ambaye nimkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Grumeti amewapongeza wazazi kwa kuwa karibu na watoto wao katika kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kutambua umhimu wa kujifunza kuhusu mazingira.

Baadhi ya wazazi na wanafunzi hao ambao wamepata fursa hiyo wamelipongeza shirika hilo huku wakisema watoto wao wamepata mwanzo Mpya wakutambua fursa nakuwa mabalozi wa badae wa mazingira kwenye maeneo yao.

Aidha Cosmas kitena na Frola Nyabokolo walisema haikuwa rashisi kuyafikia matarajio ya kutoka nje ya Tanzania kwani itawasaidia wao kufungua ukuras mpya kwenye maisha yao kupitia mazingira na ukizingatia ndio kwanza wamehimetimu kidato cha Nne

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!