Latest Posts

RAIS SAMIA ATAJA HATUA ZILIZOCHUKULIWA KULIPONYA TAIFA MBELE YA MABALOZI WA NCHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amebainisha hatua kubwa za kidiplomasia na kisiasa zinazolenga kuleta uponyaji wa kitaifa na maridhiano kufuatia misukosuko ya uchaguzi wa mwaka uliopita

Akihutubia mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa leo, Januari 15, 2026, katika hafla ya Diplomatic Sherry Party Ikulu Chamwino, Dodoma, Rais Samia amesema ametangaza msamaha kwa watu 1,787 waliohusishwa na ghasia za tarehe 29 Oktoba 2025. Hatua hiyo imetajwa kama sehemu ya mkakati wa serikali kurejesha utulivu na kuimarisha mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Katika kile kinachoonekana kama mageuzi makubwa ya kiuongozi, Rais amesema amepandisha hadhi masuala ya vijana kwa kuanzisha Wizara ya Vijana chini ya Ofisi ya Rais. Rais amesisitiza kuwa wizara hiyo mpya ina jukumu la kuratibu nguvu, ari, na matarajio ya kizazi kipya cha Watanzania ambacho ni nguzo ya maendeleo ya taifa.

“Niruhusuni nimnukuu mwanafalsafa Soren Kierkegaard, aliyewahi kusema, ‘Maisha yanaweza tu kueleweka kwa kutazama nyuma, lakini ni lazima yaishiwe kwa kwenda mbele.’ Katika muktadha huu, kama nchi, tunaelewa makosa ya huko nyuma, lakini macho yetu yamekazwa thabiti kuelekea mbeleni”, amesema Rais Samia.

Kuhusu mustakabali wa kisiasa, Rais Samia amesema ameunda Tume Huru ya Uchunguzi na kuahidi kuanzisha Tume ya Ukweli na Maridhiano, ambayo itakuwa msingi wa kuelekea mchakato wa Katiba Mpya. Amesema kuwa muhula huu wa pili utajikita katika kurekebisha, kujenga upya, na kuimarisha taifa kwa misingi ya haki na mazungumzo.

Kiuchumi, Rais amebainisha kuwa Diplomasia ya Uchumi itaendelea kuwa kiini cha sera ya mambo ya nje ya Tanzania. Amesisitiza kuwa serikali itaongeza nguvu katika uchumi wa buluu na kijani, teknolojia ya kidijitali, na usimamizi madhubuti wa rasilimali kama gesi asilia na madini ili kukuza ajira na maendeleo jumuishi kwa wote.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!