Latest Posts

SEKONDARI YA MALAMA YAPUNGUZIWA KERO YA SAMANI NA VYOO, MWASELELA AAHIDI POSHO KWA WALIMU.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela, amekabidhi msaada wa viti 200, madawati 200, na Shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Malama, iliyopo Kata ya Nsalala.

Msaada huo unalenga kupunguza changamoto ya samani katika shule hiyo yenye wanafunzi 1,589, ambapo kabla ya msaada huo ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa samani 673. Mkuu wa Shule, Neema Mwakimenya, ameeleza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kupunguza msongamano na usumbufu, hasa wakati wa vipindi vya mitihani.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mwaselela amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi. Aidha, ameahidi kuanza kuwalipa posho walimu wa kidato cha pili na cha nne wanaofundisha masomo ya ziada ili kuongeza ufaulu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa mbali ya kumpongeza Ndele Mwaselela amewataka Viongozi wa Serikali kushirikiana na jamii kuboresha miundombinu ya elimu zaidi akisema ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko wazi kuhakikisha shughuli za maendeleo haikwami.

Dinday Njile, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya amemshukuru Ndele Mwaselela kwa kuunga mkono juhudi za Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kusaidia kutatua changamoto za elimu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Akim Mwalupindi amempongeza MNEC Ndele Mwaselela kwa kukabidhi Madawati na Viti pia kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika shule ya sekondari Malama.

Akitoa taarifa ya shule Mkuu wa shule Neema Mwakimenya amesema shule hiyo yenye wanafunzi 1589 inakabiliwa na upungufu wa samani 673 hivyo vifaa vilivyotolewa na Ndele Mwaselela vimesaidia kupunguza changamoto ya samani.

Kwa upande wao baadhi ya Wanafunzi wamesema madawati na viti vitawasaidia kusoma kwa bidii kwani kipindi cha mitihani walikuwa wakichelewa kutokana na upungufu wa madati.

Shule ya Malama ni moja ya Shule za Serikali kwa sasa inakabiliwa na msongamano wa wanafunzi hivyo Kata hiyo ina mpango wa kujenga shule nyingine hii inatokana na mwitikio wa wazazi baada ya kufuta karo kwa wanafunzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!