Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Dkt. Yahaya Ismail Nawanda kama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na nafasi hiyo kuchukuliwa na Kenan Laban Kihongosi ameondolewa kutoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania iliyotolewa mapema Jumanne Juni 11, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Sharifa Nyanga imeeleza pia kuwa Rais Samia amemteua Elias Daniel Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba ambapo kabla ya uteuzi Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais Ikulu.
Hata hivyo sababu za uteuzi na utenguzi wa hivi punde haujaelezwa katika taarifa hiyo huku uapisho wa Mkuu wa Mkoa ukitajwa kuwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.