Latest Posts

OPUS YAZINDUA TUZO ZA KIMATAIFA KWA WAJASIRIAMALI

Tuzo mpya za kimataifa zimeanzishwa kutambua wajasiriamali chipukizi duniani, zikiwaandaa waanzilishi wa kampuni zilizo chini ya miaka minne na ambazo bado hazijafikia hatua ya uwekezaji wa Series A, ili kusherehekea kazi zao muhimu.

Tuzo za Wajasiriamali wa Awamu ya Mwanzo za Investec (“Investec Easies”), zinazoendeshwa na OPUS, ndizo tuzo za kwanza kubuniwa kwa ajili ya kuangazia waanzilishi wa kampuni katika hatua za awali kabisa za safari yao ya kibiashara. Wakati ambapo biashara zipatazo milioni 305 huanzishwa kila mwaka lakini ni chache hufanikiwa kuvuka mipaka, Investec Easies zimebuniwa kugundua mawazo yenye ujasiri mkubwa kabla hayajapata ukuaji mkubwa au mafanikio ya mauzo.

Kwa ushirikiano na Investec Wealth & Investment International na kampuni kubwa ya huduma za kiteknolojia iliyoorodheshwa sokoni, Endava, uzinduzi wa Investec Easies unaleta pamoja taasisi zenye ushawishi mkubwa katika mitaji na ubunifu duniani.

Washindi wa Investec Easies watachaguliwa kupitia kura za umma pamoja na jopo la kimataifa linalojumuisha wataalamu kutoka sekta za mitaji, utamaduni, na ujasiriamali.

Kwa mara ya kwanza, washindi wataungana na Ujumbe wa OPUS kuelekea Davos, hatua inayowapa fursa ya kushiriki katika jukwaa ambapo maamuzi muhimu kuhusu mustakabali wa teknolojia, tabianchi, na jamii hufanyika.

Zawadi zitajumuisha pauni 10,000 taslimu, fursa ya kuhudhuria Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) huko Davos—jukwaa ambalo kwa kawaida huhudhuriwa na makampuni makubwa, waanzilishi wa kampuni kubwa (unicorns), na viongozi wa dunia—pamoja na msaada maalumu wa kukuza biashara kutoka OPUS na washirika wake.

Mchanganyiko huu wa mtaji, fursa, na umaarufu unawapa waanzilishi nyenzo ambazo mara chache hupatikana katika hatua za mwanzo, ukiwaweka katika nafasi nzuri ya kukuza athari zao kimataifa.

Akizungumzia tuzo hizo, Sam Tidswell-Norrish, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa OPUS, alisema “Waanzilishi katika hatua hii mara nyingi hufanya kazi gizani. Katika mazingira yasiyo sawa, ni imani bila mwanga wa jukwaa inayowasukuma. Investec Easies zinatambua ujasiri wa kuanza, si uwezo wa kupanua biashara pekee. Wengi huzungumza kuhusu kampuni kubwa zenye thamani ya mabilioni, lakini kila hadithi huanza na ujasiri wa kuchukua hatua ya kwanza wazo lililoandikwa kwenye karatasi, uamuzi wa kuacha kazi salama, au usiku wa kwanza wa kukaa hadi asubuhi ukiunda programu. Hatua hizo mara chache hutambuliwa, ilhali ndizo moyo wa ujasiriamali. Kupitia Investec Easies, tunataka kusherehekea mwanga huo wa matumaini, kwa sababu ndipo mustakabali huzaliwa.”

Joubert Hay, Mkurugenzi Mtendaji wa Investec Wealth & Investment International, alisema: “Investec imejengwa juu ya misingi ya ujasiriamali — katika fikra, utendaji, na katika kujitolea kwetu kwa wateja wetu, wengi wao wakiwa ni wajasiriamali waliokomaa. Tunaamini katika thamani ya kuwekeza kwa undani katika kizazi kijacho cha wajasiriamali ambao ndio uti wa mgongo wa uchumi.

Kuna vipengele vinne vitakavyoshindaniwa ni pamoja na ImpactESEY mabadiliko yanayodumu zaidi ya mwanzilishi, ConsumerESEY chapa ambazo watu wanaamini, si tu kununua, TechnologyESEY teknolojia ambazo dunia bado haijajua kuwa inazihitaji, na FemaleFounderESEY wanawake wanaojenga kwa misingi yao wenyewe.

Naye Kristen McLeod CBE, Afisa Mkuu wa Mikakati wa British Business Bank, alisema: “Kuwaunga mkono waanzilishi wa awali ni zaidi ya kuwapatia mtaji. Tunapaswa kujenga mitandao inayoruhusu vipaji na mawazo kustawi. Mara nyingi, wajasiriamali wenye uwezo mkubwa hupitwa kwa sababu hawajapata ukubwa wa biashara au hawaonekani kama ‘wajasiriamali wa kawaida’. Hiyo ni hasara kwa jamii nzima.

Naye Alastair Lukies CBE, Afisa Mkuu wa Ushirikiano wa Endava, aliongeza kuwa: “Easies ndizo tuzo za kwanza za aina yake—zikiangaza mwanga kwa waanzilishi katika hatua za mwanzo kabisa, pale ambapo ujasiri una umuhimu mkubwa zaidi.

Maombi sasa yamefunguliwa kwa kampuni zinazoongozwa na waanzilishi ambazo zina chini ya miaka minne na hazijafikia hatua ya uwekezaji wa Series A.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 5 Novemba 2025. Orodha fupi ya wagombea itatangazwa Novemba, washindi watatangazwa Desemba, na kundi la mwisho litaungana na Ujumbe wa OPUS kuelekea Davos Januari 2026.

OPUS ni jumuiya ya kimataifa ya waanzilishi wa kampuni changa, inayowaunganisha wajasiriamali kutoka Uingereza, Afrika Kusini, na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Kwa kuchanganya teknolojia, mtaji, na utamaduni, OPUS ipo kusaidia waanzilishi kujenga biashara zenye maadili na malengo ya kimataifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!