Latest Posts

AFRICAN BOY KUWA NA KIWANDA RASMI: JUX AISHUKURU SERIKALI YA AWAMU YA SITA

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Mussa Mkambala ‘Juma Jux’, ametangaza kuanza rasmi kwa mchakato wa uanzishaji wa kiwanda cha nguo za chapa yake ya African Boy nchini Tanzania.

Kupitia ujumbe wake kwa mashabiki na Watanzania, Jux ameeleza kuwa hatua hiyo ni ushindi mkubwa kwa maono na jitihada zake katika kukuza chapa ya African Boy, huku akimshukuru Mungu kwa kufanikisha safari hiyo.

“Nina habari njema watu wangu!!! Maono na jitihada ya ‘brand’ yetu ya African Boy, hatimaye imetufikisha pakubwa leo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, mchakato wa kuwa na kiwanda chetu cha nguo za African Boy kwa hapa Tanzania umeanza rasmi,” amesema Jux.

Msanii huyo pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa usaidizi na dira kubwa ya kukuza uwekezaji, sambamba na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Bw. Gilead Teri, kwa mchango wake katika kufanikisha hatua hiyo.

“Hii ni hatua ya kuthibitisha kuwa vijana wa Kitanzania tunaweza kuwekeza, kujenga na kuamini katika nchi yetu. Safari bado inaendelea, na huu ni mwanzo tu wa kitu kikubwa zaidi,” ameongeza Jux.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kujengwa jijini Dar es Salaam, na kinaelezwa kuwa kitachangia ajira kwa vijana na kuongeza thamani ya bidhaa za nguo za Kitanzania kupitia brand ya African Boy ambayo imekuwa ikijipatia umaarufu ndani na nje ya nchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!