Kesi ya kuhoji uhalali wa tamko/ katazo la Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) lililopiga marufuku watu kutoka nje kufuatia maandamano yaliyozaa vurugu zilizopelekea uharibifu wa mali za umma na binafsi, majeruhi na vifo imeendelea leo, Alhamisi Desemba 18.2025 chini ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Immaculata Banzi, Mwanabaraka Mnyukwa na Fahamu Mtulya
Kesi hiyo, ambayo imefanyika kwa njia ya mtandao imefunguliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), ambapo leo AG na IGP wamewasilishwa na Wakili wa Serikali Waandamizi Stanley Kalokola na Wakili wa Serikali Erigh Rumisha, THBUB imewakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Rosemary Shio na TLS imewakilishwa na Mawakili Mpale Mpoki, Jebra Kambole na Hekima Mwasipu

Imeelezwa katika kesi hiyo kuwa, wajibu maombi wa kwanza na poli (AG & IGP) wameweka pingamizi moja na mjibu maombi wa tatu (THBUB) ameweka pingamizi moja, hivyo kufanya jumla ya mapingamizi mawili (2) yamewekwa na Jamhuri kwenye kesi hiyo, mapingamizi ambayo yatasikilizwa kwa njia ya maandishi kati ya Desemba 09.2025 hadi Januari 30.2026, na kwamba kesi hiyo itatajwa tena kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam Februari 09.2026, saa 03 asubuhi,
Unaweza kusikiliza zaidi hapa