Latest Posts

BILIONI 58 KIANZIO MTAJI WA BENKI YA USHIRIKA

Ujio wa Benki ya Ushirika (Coop Bank) yenye mtaji wa shilingi Bilioni 58 inatarajiwa kuwa mkombozi kwa wakulima nchini kwa kuwapa mikopo nafuu, kupanua shughuli zao za kilimo, na kuinua maisha yao kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amesema wakazi wa Dodoma watanufaika zaidi kupitia zao la kimkakati la zabibu kwa kuongeza uzalishaji na thamani ya zao hilo.

Akizungumza na wanahabari Aprili 25, 2025 ofisini kwake jijini Dodoma, Mhe. Senyamule amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa benki hiyo, utakaofanyika Aprili 28, 2025 jijini Dodoma.

“Benki hii ni ya kipekee iliyosimikwa katika misingi ya ushirika, uchumi shirikishi na maendeleo ya pamoja. Kupitia umiliki wa Hisa, kila Mtanzania anayo nafasi ya kuwa sehemu ya mafanikio ya Benki ikiwa ni chombo cha kuwezesha maendeleo ya uchumi wa watu wa kawaida” amesema Senyamule

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika (Coop Bank), Godfrey Ng’urah, amesema benki hiyo itawekeza katika teknolojia na TEHAMA ili kuboresha huduma, ambapo itazinduliwa ikiwa na mawakala 58.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!