Latest Posts

BLASISTUS NICHOLAUS ATUHUMIWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 14, ADAKWA NA POLISI

Kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Blasistus Nicholous almaarufu kwa jina la Matowa mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa mtaa wa Kitasengwa Manispaa ya Iringa anatuhumiwa kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyekuwa akifanya kazi katika duka lake.

Blasistus alikuwa akifanya kibarua Bohari ya Dawa (MSD) na kosa hilo alilifanya nyumbani kwake Kitasengwa ambapo alikuwa akiishi na kijana huyo nyumba moja.

Kwa mujibu wa mtoto aliyefanyiwa ukatili huo anasema alikuwa akiishi nyumba moja na mtuhumiwa na kulala naye kitanda kimoja ingawa nyumba yake hiyo ina vyumba kadhaa.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa iliyotolewa Alhamisi Juni 13, 2024 na ikieleza kuwa mtuhumiwa amekamatwa, Blasistus amekana kuwa hajafanya kitendo hicho ambapo uchunguzi unaendelea na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria huku taarifa hiyo ikieleza kinagaubaga juu ya tukio zima.

“Ni kwamba siku ya tukio Juni 09, 2024 majira ya saa Tano usiku huko Kitasengwa Kata ya Isakalilo Manispaa na mkoa wa Iringa kijana huyo alirudi nyumbani akitoka dukani anapouza duka la mwajiri wake ambaye ni mtuhumiwa na kwenda kulala katika chumba wanapolala pamoja siku zote tangu alipomwajiri kuuza duka hilo, Baada ya kupanda kitandani na kulala muda mfupi alisikia mtuhumiwa Blass Matowo ambaye ni bosi wake akimuita akafungue mlango ndipo alipoamka na kwenda kumfungulia na kurudi kulala, akiwa amelala kitandani alimuona mtuhumiwa anavua nguo zote na kupanda kitandani na kisha kujifunika pamoja naye” Imeeleza taarifa ya Polisi.

Taarifa ya Polisi ikaendelea kueleza bayana kuwa wakiwa wamelala pamoja mtuhumiwa huyo alianza kumvua suruali mhanga na kumuingizia ‘uume’ sehemu ya haja kubwa ambapo alihisi maumivu makali ndipo alipoinuka kitandani na kwenda kulala sebuleni kwenye kochi.

Asubuhi ya Juni 10, 2024 mwathiriwa alianza kuhisi maumivu ya tumbo na alipomaliza kuoga alijiandaa na kwenda dukani kwa bosi wake kuendelea na kazi, akiwa dukani alikuja mama yake mlezi (Mama P) na kumueleza kuwa Matowa amemfanyia kitendo hicho kibaya kisha mama huyo mlezi alienda kumueleza mume wake ambaye ni rafiki wa mtuhumiwa ndipo alipowashirikisha viongozi wa Serikali ya mtaa kwa hatua zaidi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!