Mkuu wa Wilaya ya Busega, Faidha Salim, amewataka wananchi wilayani huko kuacha kutegemea iman za kishirikina katika Kupata utajiri badala yake waelekeze nguvu katika kufanya Kazi.
Salim ametoa kauli hiyo Leo Februari 20, 2026, wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za wakulima katika kijiji cha Manara kata ya Badugu Wilayani Busega.
Akizungumza na wananchi wa Bulima katika kata ya Nyanshimo amemtolea mfano wa Mwenyekiti wa Waganga wa Tiba Asili wa Wilaya ya Busega, ndugu Peter Magubo, ambaye anajishughulisha na kilimo, unapaswa kuwa funzo kwa wengine kwani amekuwa akijishughulisha na kilimo licha ya kuwa nimganga wa Tiba Asili

“Kama Mwenyekiti wa waganga yuko shambani analima, wewe unayeenda kwa mganga unaambiwa toa kafara ili upate pesa, jitafakari,” alisema Mhe. Salim.
Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya alipata fursa ya kutembelea mashamba ya wakulima mbalimbali, akiwemo ndugu Peter Magubo, ambaye ni Mwenyekiti wa Waganga wa Tiba Asili wilayani Busega, ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kujikita katika shughuli za uzalishaji mali ili kujiletea Maendeleo zaidi.
Mhe. Salim alihitimisha kwa kuwahimiza wakulima kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa zilizopo kuboresha kipato chao badala ya kutafuta mafanikio kupitia njia zisizo na uhakika.
