Mkuu wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Thecla Mkuchika ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka na kuwchukulia hatua watu wote wanaojihusisha na kilimo cha bangi wilayani Butiama mkoani Mara baada ya kukamilisha oparesheni ya kufyeka na kuchoma zao hilo katika kijiji cha mirwa.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kukamilisha zoezi la kufyeka na kuteketeza mashamba takribani matatu yaliyokuwa yakilimwa na mwamanachi katika eneo la milimani katika kijiji cha mirwa ambapo amesema kamwe hakuna ambaye atapona atakayebainika kujihusisha na kilimo hicho.

“Kilimo hiki hakiendani nakilimo hiki wilaya hii nitakatifu niabu wananchi kulima mazao haya tunapaswa kumuenzi mwalimu katika kilimo chenye tija na skilimo hiki niwaombe wananchi watajaeni wanaofanya vitendgo hivo tutawachukulia hatua kali”Alisema Bi.Thecla Mkuchika Mkuu wa wilaya ya Butiama.
Aidha alisema kufanya oparesheni zanamna hiyo nikuwasaidia wananchi kujiepusha na kilimo pamoja na matumizi ya zao hilo huku mmoja ya wananchi waliokutwa katika eneo hilo walitaka wananchi wenzao kuachana na kilimo cha namna hiyo.