Latest Posts

DKT. SAMIA AAHIDI UJENZI WA BARABARA NA MASOKO ARUMERU ENDAPO ATAINGIA MADARAKANI

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema endapo atapewa nafasi ya kuunda serikali katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, serikali yake itatekeleza miradi ya ujenzi wa barabara na masoko katika Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha.

Akihutubia wananchi leo Jumatano, Oktoba 1, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Kituo cha Mabasi Usa River, Dkt. Samia ametaja barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami kuwa ni Malula–Ngarenanyuki (km 33.7), Tengeru–Usa River (km 11.3) na Maji ya Chai–Sakila (km 16).

“Serikali ya Chama Cha Mapinduzi tupo hapa kuomba kazi, tupeni kazi tukatekeleze miradi na mambo mbalimbali yanayokwenda kuutukuza na kuuheshimisha utu wa Mtanzania kupitia maji, umeme, afya, barabara na huduma nyingine,” amesema Dkt. Samia.

Mbali na miradi ya barabara, amebainisha kuwa serikali yake pia itatekeleza ujenzi wa soko la Ngaramtoni na kuendelea na mpango wa ujenzi wa soko la Tengeru katika kipindi cha miaka mitano ijayo, endapo atapewa ridhaa na Watanzania kuiongoza tena serikali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!