Latest Posts

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amefika Wilaya ya Monduli kunusuru bwawa la Nanja ambalo ni tegemeo la vijiji 30 katika chanzo maji pekee.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amefika Wilaya ya Monduli kunusuru bwawa la Nanja ambalo ni tegemeo la vijiji 30 katika chanzo maji pekee, baada ya kumeguka kingo zake kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. Amesisitiza kwamba pamoja na ugumu wa kukarabati bwawa hilo wakati likiwa na maji, maamuzi magumu yafanyike kwa wataalamu wa Wizara ya Maji kutumia utaalamu wao kulifanikisha hilo kwani hakuna namna nyingine. Akizungumza na mamia wa wananchi wa kata za Lepruko, Sepeko, na Makuyuni, Aweso ameelekeza wataalamu wa wizara kutumia taaluma zao kuhakikisha bwawa hilo linakarabatiwa kwa dharula ili kudhibiti maji kuendelea kupotea Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Monduli Fred Lowassa, amesema bwawa hilo ni tegemeo la Wanamonduli kwenye matumizi ya maji kwa binadamu, mifugo na wanyamapori, hivyo anaiomba serikali ione namna ya kukarabati bwawa hilo kwa dharura. Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti madiwani wa kata zinazoguswa na bwawa hilo, wameishukuru serikali kwa kuwafikia kwa haraka na kutafuta suluhu ya changamoto inayowakabili.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!