Latest Posts

FAMILIA NI MSINGI WA HAKI NA USTAWI, TUZILINDE- MHE. MTAMBULE

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar Es Salaam Mhe. Saad Ahmed Mtambule amesisitiza Waislamu na Watanzania wote kwa Ujumla kurejea katika misingi na maadili ya Kitanzania kwa kuimarisha familia na kulea Vijana katika maadili na utamaduni wa Kitanzania.

Mhe. Mrambule amebainisha hayo leo Jumamosi Disemba 27, 2025 wakati wa kongamano la dini Jijini Dar Es Salaam, akisisitiza kuwa familia ndiyo msingi wa haki na ustawi wa watu na Taifa kwa ujumla, hivyo ni muhimu kuwekeza katika familia na maadili ya Mtanzania katika kukuza jamii.

“Chakula kikuu cha amani ni sisi binadamu na sisi chimbuko letu si chama cha siasa ama ofisi fulani. Chimbuko letu sisi ni Familia kama Taasisi ya kwanza ya binadamu. Familia ni msingi wa amani, msingi wa haki na msingi wa ustawi wa Taifa lolote lile.”Amesema Mhe. Mtambule.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mtambule amebainisha kuwa ikiwa ataonekana mtu asiyefuata maadili, mwenye kuendekeza vitendo vya rushwa, ubadhirifu na kutowajibika vyema ni kushindwa kwa Taasisi familia, akisema kabla ya shule, vyama vya siasa na Taasisi za kidini ni muhimu kutambua umuhimu na nafasi ya familia katika malezi na kumtengeza raia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!