Latest Posts

GRUMETI FUND YAWAJENGEA UWEZO VIJANA 100 KUPAMBANA NA UKOSEFU WA AJIRA

Zaidi ya vijana 100 wanaofadhiliwa kimasomo na shirika la Grumeti Fund kutoka vijiji 22 vilivyopo wilayani Serengeti na Bunda Mkoani Mara wamepatiwa mafunzo na mbinu bora za kujitegemea na kukabiliana na changamoto za kimaisha kwenye maeneo yao pamoja na kupoambana na changamoto ya ukosefu wa ajira badala yake vijana hawa wameze kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao kuchangamkia fursa.

Akizungumzia mafunzo hayo Afisa Elimu ,Idara ya maendeleo ya jamii kutoka Grumeti Fund Elizabeth Magoto alisema  kuwa shirika hilo mbali na kutoa elimu ya stadi za maisha limekuwa  likiwasaidia  vijana katika kuwapatia ufadhili wa kimasomo pamoja na kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitambua ,stadi za biashara,teknlojia  na mawasiliano bora sambamba na usimamizi wa fedha .

“Tumekutana na vijana zaidi ya 100 lengo likiwa ni kufundisha stadi za maisha kwani zipo stadi ambazo vijana wanatakiwa kuwa nazo lakini hazifundishwi mashuleni hivyo Grumeti Fund tunaamini kuwa kwa kuwajengea vijana msingi imara wa stadi za maisha, tunatengeneza jamii yenye uelewa mpana ambayo inaweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo bila utegemezi” alisema Bi. Elizabeth

Pia  Elizabeth amebainisha kuwa programu hiyo  ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Shirika hilo kutengeneza kizazi cha vijana chenye kujiamini, kujitambua sambamba na kupambana na umaskini na ukosefu wa ajira kwani kupitia mafunzo haya vijana wanakuwa na ujasiri wa kuanzisha miradi midogo midogo ya ujasiriamali.

Naye Afisa Miradi Grumeti Fund Idara ya Maendeleo ya Jami Ndg. Philip Kitasho, amewataka vijana walionufaika na mafunzo hayo, kutumia muda wa likizo kuanzisha biashara ndogondogo huku wakitumia ujuzi waliopata katika mafunzo jambo ambalo litaounguza utegemezi wao kwa wazazi na kuwataka kusambaza ujuzi huo kwa vijana wengine ili jamii nzima iweze kunufaika.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamelishukuru Shirika la Grumeti Fund kwa elimu hiyo huku wakiaidi kuyaweka katika vitendo yote waliyofundishwa na kuwa mabalozi wema wa mabadiliko katika jamii zao, wakitumia maarifa waliyopata kujenga maisha bora na yenye tija kwa ajili ya mustakabali wa jamii zao na Taifa kwa ujumla.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!