Latest Posts

HUKUMU NZITO TANGA: KIFUNGO CHA MAISHA NA MIAKA 30 KWA KUBAKA NA KULAWITI

Mahakama ya Wilaya ya Tanga mkoani Tanga imemhukumu Charles Felix (26), mfanyabiashara na mkazi wa Donge, kutumikia kifungo cha maisha jela pamoja na kifungo cha miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya kubaka na kulawiti msichana mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Chuda.

Hukumu hiyo imetolewa Julai 22, 2025 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tanga, Mheshimiwa Kobero, ambaye amesema mahakama imejiridhisha kuwa upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha, usioacha shaka dhidi ya mshtakiwa.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Jeshi la Polisi la Tanzania, tukio hilo lilitokea mnamo Juni 28, 2024 katika maeneo ya Chuda, ambapo mshtakiwa alifanya vitendo hivyo kwa nyakati tofauti dhidi ya binti huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kisheria.

Kesi hiyo, yenye namba ya jinai 27451 ya mwaka 2024, iliripotiwa na Sara Luono, mama lishe na mkazi wa Chuda, ambaye aliwasilisha taarifa kwa vyombo vya usalama. Uchunguzi uliofanywa na polisi ulisababisha mshtakiwa kufikishwa mahakamani na hatimaye kuhukumiwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!