Latest Posts

IGP: TUSIKUBALI KUGAWANYWA KWA SABABU YOYOTE ILE

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amewataka Watanzania kutokubali kugawanyika kwa sababu yoyote ile, iwe ya kidini, kisiasa au rasilimali na badala yake waendeleze upendo na amani ya taifa.

IGP Wambura aliyasema hayo Novemba 21, 2025 wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Askari Polisi Kozi Namba 1/2024/2025 katika Shule ya Polisi Tanzania – Moshi, Kilimanjaro.

IGP Wambura amesema amani ya nchi ni jambo la muhimu hivyo kila mmoja anawajibu wa kuendeleza amani na usalama wa nchi ambayo imedumu kwa muda mrefu tangu tumepata uhuru.

Pia, amewataka watanzania kuendeleza ushirikiano, umoja na mshikamano na Jeshi la Polisi kwa maslahi ya taifa letu.

Aidha, IGP Wambura amewataka askari wahitimu kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyojifunza kwa kuhakikisha kuwa wanaimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu.

Vilevile, amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuendelea kutoa ajira ndani ya Jeshi la Polisi pamoja na kuboresha vitendea kazi, makazi, ofisi na kuboresha maslahi ya askari Polisi.

Jumla ya Askari 4826 wamehitimu mafunzo hayo ya awali yaliyodumu kwa muda wa miezi kumi na mbili ambapo wahitimu hao wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!