Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi imemteua Issa Juma Ngasha kugombea nafasi ya udiwani katika Kata ya Ng’apa, Manispaa ya Lindi.
Uteuzi huo umetangazwa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Lindi, Patrick Magarinja, ambaye alieleza kuwa Ngasha aliongoza kura za maoni kwa kupata kura 183, akimshinda diwani aliyemaliza muda wake aliyepata kura 114.
Kata ya Ng’apa sasa inajiandaa kwa mchakato wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, mwaka huu, ambapo uteuzi wa Ngasha unaelezwa kuungwa mkono na wanachama wengi wa chama hicho.