Theophilida Feliacin, Kagera.
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mhe Stephen Byabato ameipongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kukitatua kilio cha wananchi wa jimbo la Bukoba mjini baada ya kuanzisha ujenzi wa miradi mikubwa mitatu yenye zaidi ya Sh Bilioni 40.
Byabato ameyaeleza hayo akiwahutubia wananchi katika hafla fupi ya kuwakabidhi mikataba ya kuanza ujenzi wakandarasi shughuli iliyofanyika eneo la soko kuu la zamani mjini Bukoba.
Ameitaja miradi hiyo ni pamoja na kituo kipya cha mabasi Kyakailabwa, soko kuu la kisasa na kingo za mto Kanoni miradi ambayo itakuwa yenye manufaa kwa wananchi wa Bukoba na mkoa kwa ujumla.
Amefafanua kwamba miradi hiyo nisehemu ya maombi aliyoayandika kwa serikali lengo kuinua maendeleo ya Bukoba na baada ya taratibu kufanyika serikali imejibu maombi hayo na miradi tayari inaanza ujenza ndoto ambayo niya muda mrefu kwa wakazi wa bukoba.
Amewashukuru viongozi wote walioungana naye katika kuihangaikia miradi hiyo bila kuwa sahau wananchi ambao wamekuwa naye bega kwa bega na matunda yamaendeleo yanaendelea kustawi kwa kasi hivyo amewaomba kuendelea kuwa wamoja hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu huku akisikitishwa na hali ya siasa zenye viashiria vya chokochoko zilizoanza kuchomoza dhidi yake.
Mkuu wa mkoa Kagera Mhe Fatma Mwassa akiwa mgeni rasmi awali ameanza kuishukuru serikali kwa miradi hiyo ambapo amewataka wakandarasi kuijenga kwa wakati ndani ya muda wa miezi 15 kama yalivyo maelekezo ya mkataba.
Amewataka wananchi kuilinda miradi ili kuwawezesha wakandarasi kwenda kasi bila mkwamo kama yalivyo makundi ya serikali.