Latest Posts

MAELFU WASHIRIKI ‘GENERATION SAMIA JOGGING’ DODOMA

Maelfu ya vijana wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika tukio la Generation Samia Jogging lililofanyika jijini Dodoma, wakionesha mshikamano wa dhati na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Generation Samia Jogging imefanyika Desemba 7, 2024 ikivuta hisia za wengi na kuwa nembo ya mshikamano wa kizazi kipya kwa kudhihirisha jinsi vijana wanavyothamini na kuunga mkono dira ya maendeleo ya serikali.

Wakiwa na ari na nishati, washiriki walionekana wakishiriki mbio hizo kwa furaha, huku wakitoa ujumbe wa mshikamano wa kitaifa.

Kwa mujibu wa waandaaji, mafanikio makubwa ya tukio hili yanaashiria azma ya vijana kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kushiriki agenda za maendeleo ya taifa.

Aidha, wameahidi matukio zaidi ya aina hii yatakayolenga kuimarisha mshikamano wa kijamii, kukuza ari ya kizalendo, na kuhamasisha jamii kuishi kwa mtazamo chanya wa maendeleo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!