Latest Posts

MKOA WA MARA WAPOKEA MAGARI MATATU KUTOKA AMREF

Magari matatu yamekabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na Musoma mkoani mara na Shirika la Amref Tanzania kwaajili ya ufuatiliaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kupokea magari hayo kutoka kwa Meneja Miradi wa shirika la Amref Tanzania Dkt. Recotus Masanja, Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Gelard Kusaya amewaonya madereva kuacha kupakia vitu visivyostahili katika magari hayo badala yake yatumike kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Zabron Masatu amesema kupatikana kwa magari hayo kutasaidia kuondoa changamoto ya ukosefu wa magari huku Meneja Miradi wa Amref akisema magari hayo yametolewa ili kusaidia utoaji wa huduma kwa wananchi na si vinginevyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!