Latest Posts

MTWARA WAHIMIZWA KULITANGAZA TAMASHA LA NYANGUMI

Wananchi mkoani Mtwara wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara yanapotokea matamasha na shughuri mbalimbali zinazokusanya watu wengi ili waweze kujiingiza kipato.

Hayo yamezungumzwa Septemba 7,2024 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Selemani Nampanye kwenye kilele cha Tamasha la Nyangumi lililofanyika kwenye kata ya Msimbati Halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Amesema kupitia matukio ya aina hiyo kuna fursa mbalimbali ambazo wananchi wanapaswa kuzichangamkia kwa kujiongezea kipato.

Aidha amewaomba wananchi hao kuendelea kulitangaza na kulipa uzito mkubwa tamasha hilo la nyangumi Festival kwa ajili ya maslahi makubwa ya mkoa na Tanzania kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kushiriki kikamilifu kwenye matamasha kama hayo ili waweze kutoa huduma ya elimu kwa mwananchi kupitia majukwaa hayo lakini pia kudhamini ili tamasha hilo liweze kufanyika kwa ukubwa zaidi.

“Niwakalibishe taasisi zote za umma na binafsi zinazoweza kudhamini matamasha kama hayo ili yaweze kufanyika kwa ukubwa na ubora wa kitaifa na zilete tija zaidi ya kiuchumi kwa wananchi wetu,natamani nione tamasha hili mwakani linafanyika kwa ukubwa zaidi na kuwa na sura ya kitaifa.”amesema Sawala.

Ameongeza kuwa uchumi wa Mtwara unategemea sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, uvuvi, mifugo na biashara ambapo kwasasa sekta ya utalii nayo inakwenda kuwa tegemeo la kuongeza uchumi wa mtwara hivyo amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kuongeza uchumi wao familia,Wilaya na mkoa mzima.

Kwa upande wao mashuhuda ambao wamefanikiwa kushuhudia nyangumi hao wamesema utalii huo ni mkubwa kwa kutangaza mkoa ikizingatiwa nyangumi hapatikani kokote nchini Tanzania.

Jamali Andenani amesema “Kimsingi ni uaminifu kwamba hivi viumbe vipo duniani lakini pia vipo katika bahari yetu ya mtwara kwasababu wengi tunaamini tunapewa tu promotion kuwa Mtwara kuna nyangumi ila leo hii kupitia hii festival tumejionea wenyewe.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!