Latest Posts

MUSSA KIDATO ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE HANDENI

Mwanadiplomasia wa Uchumi, Mtaalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), na Mtaalam wa Hali ya Hewa, Mussa Kidato, ametangaza nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Handeni kwa lengo la kuwatumikia wananchi kwa ufanisi na kuendeleza juhudi za maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Kidato, ambaye pia ni mwanasiasa mkongwe ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), anatajwa na wakazi wa Handeni kuwa ni mtu sahihi kwa wakati huu, kutokana na rekodi yake ya kujitolea, uchapakazi, na uzoefu wa kisiasa uliotandaa kwa zaidi ya miongo miwili.

Kidato si jina geni kwa wakazi wa Handeni. Anakumbukwa kwa ujasiri wa kuanzisha miradi ya kijamii tangu miaka ya 90, ikiwa ni pamoja na kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuanzisha huduma za usafiri wa abiria Handeni mjini, kwa mfumo wa “safiri kwanza, lipa ukifika”, pamoja na kuleta mashine ya kwanza ya kusaga katika eneo hilo.

Kwa upande wa chama, amewahi kuwa Kiongozi wa UVCCM Tawi (1997), Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM (2004), Mjumbe wa TUGHE Tawi la Makao Makuu (2005), Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Handeni (2017), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Handeni (2017) na Msaidizi/Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (2019).

Katika nafasi hizo, Kidato amekuwa kiungo muhimu kati ya wananchi na taasisi mbalimbali, akiwasemea vijana, akisaidia kuhamasisha miradi ya TEHAMA, mazingira na elimu ya hali ya hewa vijijini.

Kidato amesema yupo tayari kushirikiana na wananchi wa Handeni ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia ushirikiano na sekta binafsi kwa ajili ya ajira kwa vijana, Mipango ya TEHAMA kwa elimu na kilimo, kuibua miradi ya vyanzo vya maji, barabara na afya, na kujenga Handeni ya kisasa kupitia maendeleo ya kiuchumi yanayogusa maisha ya kila mmoja

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!