Latest Posts

ORYX ENERGIES YAZINDUA MFUMO WA KWANZA WA GESI YA LPG KWA WINGI SOKO LA SAMAKI FERI

 

KAMPUNI ya ORYX Energies Tanzania kwa kushirikiana na Serikali na wadau wa soko, wamezindua mfumo wa kwanza wa usambazaji wa gesi ya LPG kwa wingi katika Soko la Samaki la Kimataita Ferry jijini Dar es Salaam ambapo unakwenda kuimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa wauzaji wa samaki na wajasiriamali wadogo katika soko hilo.

Mfumo huo unaweza kulipia kadri ya matumizi (PAYG), unaowawezesha wauzaji kulipia gesi wanayotumia tu na hivyo kuondoa gharama kubwa za kujaza mitungi na kupunguza matumizi ya kila siku hadi Sh.45,000.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo huo ambapo limejengwa tanki kubwa ambalo linatumika kusambaza gesi katika majiko ya wafanyabiashara hao,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema mfumo huo sasa utawezesha kulipa kulingana na matumizi yako.

Chalamila amesema kuwa ajenda ya kuwa na matumizi ya nishati safi ya kupikia ilikuwepo tangu zamanı lakini mkazo wake ulikuwa mdogo lakini Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameibeba ajenda hiyo na Oryx Energies wameonesha kwa vitendo kuunga mkono jitihada hizo kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.

“Wenzetu Oryx Energies kwa kuendelea kujitoa kwao katika eneo hili la nishati safi ya kupikia kwa kuja na Mfumo huu ambao sasa unakwenda kurahisisha upatikanaji gesi katika soko hili la samaki feri.

“Hapa katika Soko la samaki feri kuna majiko ya wakaanga samaki 48 na sasa wote wameunganishwa katika mfumo huo wa gesi na tunaamini matumizi ya nishati safi ya kupikia yanakwenda kuokoa hata changamoto za kiafya za watumiaji wakiwemo wanawake ambao wanafanya shughuli zao katika soko la samaki feri .

Amefafanua matumizi ya nishati safi ya kupikia hayaokoi tu afya za watumiaji bali hata gharama za uendeshaji zinapungua kwa asiliamia kubwa na kuongeza mradi huo umegharimu zaidi ya Sh.milioni 250 na
matamanio yake ni kuona masoko yote yalipo katika Jiji la Dar es salaam yanakuwa na mfumo huo.

Chalamila amewataka wadau wote wanishati safi kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hususan kwa kuyafikia masoko yote lengo nikuona afya za watu zinakwenda kuwa salama .

Akieleza zaidi amesema leo hawazindui tu miundombinu bali wamezindua mabadiliko ya kweli katika usalama, ufanisi, na ustawi wa kila mfanyabiashara anayefanya kazi hapa sokoni.Kupitia mradi huo Oryx wameweka matanki ya gesi chini ya ardhi, vaporizers, na mtandao wa mabomba unaohudumia majiko yote 48

Amesema kila mfanyabiashara sasa ana mita yake inayosoma matumizi yake ya kila siku, kabla na baada ya matumizi. Hakuna tena kubahatisha, hakuna tena kulazimika kununua mitungi midogo kwa gharama kubwa.

Pia amesema Oryx wamezingatia usalama,kwa kufunga valve ambazo itatumika kufunga gesi endapo itatokea dharulakwa kila jiko. Tunafahamu matumizi makubwa hivi ya gesi yanahitaji usalama wa hali ya juu.

“Nafahamu kwamba Oryx mtaendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya huu mfumo ilikuepusha ajali yoyote inayoweza kutokea kwa kutokujua aukupuuzia kanuni sahihi za usalama. Nimeambiwa pia kuwa mradi huu ni ufadhiri wa asilimia 100 toka kwenu Oryx energies na mmetumia zaidi ya TZS milioni250.

“Tunawashukuru kwa imani yanu katika jamii kwa kujitoleakuleta nishati salama na endelevu. Mmemuunga mkonoMheshiwa Raisi wetu kwenye mambo mengi hususani katikasecta hii ya nishati safi na hii ya leo mmezidi kudhihirishadhamira yenu njema katika kuwainua Watanzania kuhamia matumizi ya nishati safi ya kupikia.”

Akifafanua zaidi amesema kuwa faida za matanki ya gesi yaliyofungwa yanaondoa usumbufu wakubadilisha kubadilisha ile mitungi midogo midogo mara kwa mara,gesi pia itapatikana inapatikana bila usumbufu.

Pia amesema viwango vya matumizi gesi vitafuatiliwa kwa urahisi ili kuhakikisha gesi inaletwa kujaza kwenye hili tanki kubwakwa wakati huku akieleza gharama imepungua na wafanyabiashara waliokuwa wakitumia hadi Sh.180,000 kujaza gesi kwa siku sasa wanaweza kuokoa hadi Sh.45,000 kila siku.

“Kupitia mfumo wa Lipa Kadri Unavyotumia,hili ni suala la kupongezwa sana.Hakuna upotevu, hakuna gesi isiyotumika tofauti na zamani ambapo mtungi mdogo mliotumia wakati fulani gesi inabaki kidogo. Usalama wa Juu, hili sina shaka na utalamu wenu Oryx kwenye suala zima la usalama.Nafahamu tahadhari zote zimezingatiwa hasa kwa kuweka Vifaa vya kuzima moto nataratibu za dharura zipo tayari.

“Huu si tu mradi wa kiufundi bali ni mradi wa kibinadamu. Hasa pale unapowazezesha wafanyabiashara kwa vitendea kazi ili kufanikisha kazi zao, mazingira salama ya kufanya biashara, nauhuru wa kuzingatia kile wanachokifanya kwa ufanisi mkubwa

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Benoit Araman amesema lengo la kuwa na mfumo huo wa kuwa na tanki la gesi katika soko hilo unalenga kupunguza gharama za kujaza, kupunguza upotevu, na kuongeza ufanisi
Usalama Mfumo usiovuja

Amesema ni mfumo wa kisasauliofanywa na team ya ufundi ya Oryx gas kwa kuzingatia kanuni za kitaifa na kimataifa.Pia urahisishaji wa Uendeshaji Ugavi endelevu pamoja na ufuatiliaji wa kisasa, na matengenezo madogo.

Kuhusu Dira ya Taifa Kupanua matumizi ya nishati safi Benoit amesema ORYX Energies imejipanga kuunga mkono Mkakati wa Taifa wa Kupikia kwa Usafi 2024–2034, kwa kusambaza mfumo huu katika masoko ya samaki ya Zanzibar, Mwanza, na mikoa mingine.

“Kampuni pia inaendelea kuunganisha hii mifumo ya LPG kwa wingi pia mashuleni, taasisi, majengo ya biashara, naviwanda kote nchini.Mradi huu si miundombinu tu ni ahadi ya kuinua jamii, kulinda mazingira, na kuchochea ukuaji wa uchumi,” alisema.

Awali Kamishina wa Nishati Mhandisi Innocent Luoga kutoka Wizara ya Nishati ameeleza hatua mbalimbali ambazo zinaendelea kuchukuliwa na Serikali katika kufanikisha mpango wa nishati safi huku akiiipongeza Oryx kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Tangu mkakati wa kitaifa ulipozinduliwa Januari mwaka 2024 wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kumekuwepo na mafanikio makubwa na ongezeko la matuminizi ya majiko ya gesi yamekuwa makubwa,”amesema Mhandisi Luoga na kufafanua mkakati wa Serikali ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

” Ili kufikia malengo hayo mkakati ni kwamba taasisi,au makundi makubwa yanayolisha watu kwa pamoja wanahamia katika Matumizi ya Nishati safi ya kupikia na katika hili maeneo mengi tayari yameaza kufikiwa.

Katika hatua nyingine aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Ilala Dar es Salaam Mussa Zungu amesema awali wafanyabiashara wa soko hilo walimfikishia mahitaji yao hivyo aliwatafuta Oryx Gas na leo amefurahi kuona umefungwa mfumo huo ambao unakwenda kurahisisha shughuli za wafanyabiashara hao.

Zungu amesema tafiti zinaonesha duniani kuwa Kuna vifo vingi vinavyotona na Matumizi ya Nishati isio salama hivyo Mradi huu unakwenda kuwa majawabu ya kuimarisha Afya za wadau hao.”Lengo nikufanya biashara kwa amani katika eneo hili lakini ametaka kuendelea kutoa elimu juu ya Mradi huo.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!