Latest Posts

RC CHALAMILA: WAFANYABIASHARA WALIOFUNGUA MADUKA KARIAKOO WASISHINIKIZWE KUFUNGA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila Jumatatu Juni 24, 2024 amefika eneo la Kariakoo maarufu kwa shughuli mbalimbali za kibiashara jijini humo kwa lengo la kujionea hali halisi kufuatia mgomo wa wafanyabiashara ambapo amejionea baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa na mengine yamefunguliwa.

RC Chalamila amesema eneo hilo lina amani na usalama wa kutosha ambapo amewataka wafanyabiashara waliofungua maduka kuendelea kufanya biashara kwa uhuru na kwamba asitokee yeyote wa kushinikiza waliofungua maduka wayafunge.

Aidha RC Chalamila amesema falsafa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kutatua migogoro kwa kukaa mezani na kuna juhudi zinafanyika kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo ambapo amesema kuwa viongozi wa wafanyabiashara tayari wako Dodoma kwa lengo la kupata suluhu za changamoto za wafanyabiashara hivyo kufunga maduka ni kukosa uvumilivu.

Vilevile RC Chalamila ametoa rai kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kutatua migogoro kwa kukaa mezani pamoja na serikali badala ya kuweka mashinikizo ambayo yanaweza kupelekea vurugu na kuhatarisha amani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwisho RC Chalamila amewahakikishia wafanyabiashara wote wa Kariakoo waliofungua na waliofunga maduka kuwa eneo hilo ni salama salimini likiwa na ulinzi wa kutosha hivyo wanaofanya biashara waendelee kufanya biashara zao kwa uhuru.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!