Latest Posts

RC MARA AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI KUKABILIANA NA MATUKIO YA UKATILI

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuchukua hatua kali kudhibiti vitendo vya ubakaji na ukatili wa kingono unaoendelea kujitokeza katika kata ya Nyamwaga, wilayani humo.

Kanali Mtambi ametoa agizo hilo wakati akikagua ujenzi wa jengo la linalogharimu kiasi cha shilingi milioni 189, linalojengwa kwa ajili ya kudhibiti ukatili wa kijinsia, jengo lililopo katika kituo cha afya Nyamwaga.

Amesema yapo matukio kadha wa kadha katika eneo hilo ikiwamo matukio ya ukatili wa kingono hususani kwa watoto wadogo ambapo ameagiza hatua kali kuchukuliwa ili kukomesha tatizo hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Maulid Surumbu amesema kwa sasa baadhi ya ng’ariba waliokuwa wanaojihusisha na vitendo vya ukeketaji wanadaiwa kubadili mbinu baada ya kuanza kuwatumia wakunga wajadi katika kutekeleza jambo hilo.

Naye, Afisa ustawi wa jamii katika kituo cha afya Nymwaga Adecoda Joseph amesema ukatili wa wanaume kutekelezwa ni miongoni mwa ukatili unashamili katika eneo hilo kwa sasa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!