Latest Posts

RC MTAKA: MMEZOEA MIUJIZA,SASA TUNA WIKI YA MATIBABU KISAYANSI MTOKE MAJUMBANI

Njombe.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kufanya vipimo na kupata matibabu ili kuimarisha afya itakayowezesha wananchi wa mkoa huo kuendelea kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujitafutia kipato wakiwa na afya njema.

Mtaka ameeleza hayo kwa wananchi mkoani humo mbele ya balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian alipotembelea shughuli za utoaji wa huduma ya matibabu ya kibingwa bure kupitia kwa madaktari bingwa kutoka China, huduma zinazotolewa katika kituo cha zamani cha mabasi Njombe Mjini.

“Watu wamezoea kuambiwa miujiza na mnaacha shughuli zenu sasa tuna wiki ya matibabu ya kisayansi tokeni majumbani mje mfanye vipimo na matibabu ili uweze kutengeneza mtaji wa afya yako kwa kuwa utafanya biashara lakini utahitaji afya na tuna shida sana ya wafanyabiashara wetu wengi wanakufa vifo vya ghafla wanadhani kwamba wamerogwa sasa Clinick iko hapa tumieni fursa uje hapa”, amesema Mtaka.

Naye Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema China ni nchi pekee duniani iliyofanikiwa kufikisha timu ya wataalamu wa afya kwenye nchi nyingine kwa muda mrefu hivyo pia kutokana na uhusiano wa muda uliopo baina ya Tanzania na China wataendelea kushirikiana katika nyanya mbalimbali ikiwemo kwenye sekta hiyo ya afya.

Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Juma Mfanga amesema miongoni mwa huduma za matibabu ya kibingwa yaliyoletwa na Ubalozi wa China na kutolewa bure ni pamoja na uchunguzi na matibabu ya moyo, uchunguzi na matibabu ya mifupa na viungo, uchunguzi na matibabu ya ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu,Uchunguzi na matibabu kwa wagonjwa mahututi pamoja matibabu ya usingizi na ganzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!