Latest Posts

RC MTWARA AAGIZA TANROADS KUONGEZA KASI YA UJENZI MNIVATA–MITESA

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota, amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kutoa azimio kuhusu changamoto za ujenzi wa barabara ya Mnivata hadi Mitesa, ambazo kwa kiasi kikubwa zinawaathiri watumiaji wa barabara hiyo.

Chikota ametoa ombi hilo katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Mtwara, kilicholenga kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za miundombinu ya barabara ambapo amesema barabara hiyo ina changamoto kubwa ya barabara za mchepuo (diversion), hali inayosababisha magari kukwama na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Hassan Salamata, amesema kuwa barabara nyingi hazina mifereji ya maji, hivyo mvua zinaponyesha barabara hizo huwa hazipitiki.

Akitoa ufafanuzi kuhusu changamoto ya barabara za mchepuo katika ujenzi wa barabara ya Mnivata hadi Mitesa, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mtwara Emily Zengo, amesema kuwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo, tayari wamemwondoa msimamizi mkuu wa mkandarasi na kumleta msimamizi mwingine ili kuongeza ufanisi,

Ameeleza pia kuwa kuhusu changamoto ya barabara za mchepuo, TANROADS wamemuelekeza mhandisi mshauri kumkata mkandarasi fedha zinazohusiana na ujenzi wa barabara hizo, ili kutafuta wazabuni wengine watakaofanya kazi hiyo kwa ubora unaotakiwa.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ameiagiza TANROADS kumsimamia kikamilifu mkandarasi ili aongeze kasi ya ujenzi, pamoja na kuhakikisha barabara za mchepuo zinapitika wakati wote wa ujenzi, hususan katika kipindi cha masika, kwani kwa sasa hazijajengwa kwa ubora unaokubalika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!