Theophilida Felician , Kagera.
Maisha magumu, upweke, migogoro ya ndoa, wivu wa mapenzi, madeni makubwa, msongo wa mawazo, ulevi uliopindukia na ramli chonganishi ni miongoni mwa sababu zinazochangia kasi ya matukio ya watu kujitoa uhai kwa kujinyonga.
Kauli hiyo imetolewa na mchungaji wa kanisa la EAGT MLIMA WA AHADI Clavery Venant wakati akizungumza na Blog hii ofisini kwake manispaa ya Bukoba ambapo amesema kutokana na jamii kukabiliwa na changamoto mbalimbali watu wamekuwa wakukata tamaa na matokeo yake kuchukua maamuzi yasiyo sahihi hususani ya kujiua matukio ambayo yameshika kasi kutokana na kuripotiwa mara kwa mara maeneo mbalimbali nchini.
Amefafanua kuwa kujiua siyo maamzi sahihi ni maamzi mabaya kwani hali hii imepelekea athari ya kuwapoteza watu wanaoziacha familia zikitangatanga kwa jamii hasa watoto yatima.
Mchungaji huyo amesema tatizo hilo limewakumba hata watoto wadogo kuchukua maamuzi hayo ya kujinyonga moja ya sababu ikiwa ni kutokupata malezi ya upendo wa dhati kwa wazazi kwani wazazi wamejisahau katika eneo hilo badala yake watoto wanajikuta wakilelewa na watu wengine wakiwemo ndugu wa familia na wafanya kazi wandani jambo ambalo limewapelekea baadhi yao kukutwa na ukatili dhidi ya vitendo vya ubakaji.
Ametoa wito kwa jamii kuachana na vitendo hivyo viovu wawashirikishe watu changamoto zao ili kupata ushauri pamoja na kumcha Mungu yeye atawaponya makovu ya maumivu yaliyoighubika mioyo yao huku akiwasihi kutokutenda dhambi.
Hata hivyo amewashauri viongozi wa dini, wanasaikolojia na makundi mengine kujitokeza na kuwasaidia wananchi kuwapa elimu yenye ufahamu juu ya madhara ya kujiua itaweza kuyapunguza na kuyadhibiti matukio ya namna hiyo kwa jamii.