Latest Posts

SANGU: BODI YA WADHAMINI WCF KUTEKELEZA DIRA 2050

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) imetakiwa kuweka mikakati ya kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili mfuko uchangie katika kutoa huduma bora zaidi ikiwemo kuongeza uzalishaji ajira kwa sekta binafsi.

‎Sangu amesema serikali kupitia Dira 2050 inalenga kuanzisha na kuimarisha mfumo jumuishi wa Hifadhi ya jamii ili kujumuisha sekta isiyo rasmi katika mfumo wa Hifadhi ya jamii hatua itakayochochea uwekezaji wa miradi ya maendeleo na  uzalishaji ajira kwa watanzania wengi zaidi.

‎Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Deus Sangu wakati alipofanya kikao na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya WCF jijini Dodoma.

‎Waziri Sangu amewaeleza wajumbe hao kuwa Serikali kuanzia mwezi Julai mwaka huu itaanza utekelezaji wa Dira 2050 ambapo kwa sekta ya hifadhi ya jamii dhima mojawapo ni kuhakikisha ukuaji wa Uchumi Jumuishi na uzalishaji wa ajira unapewa kipaumbele kupitia sekta binafsi.

‎Waziri huyo ameongeza kusema katika mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano utakaochangiwa sekta binasfsi inatakiwa kuchangia asilimia 70 ambapo Mfuko wa WCF unatakiwa kuongeza wigo wa kuandika wanachama toka sekta binafsi ili kiwango cha uchanguaji kikue zaidi.

‎“ Tuitazame sekta binafsi kama kiungo cha kukuza Uchumi ambapo mfuko wa WCF unapaswa kubuni na kuwekeza kwenye miradi ya kimakakati ambayo itaongeza kasi ya uzalishaji ajira ili mfuko upate wachangiaji wengi zaidi na kuufanya uendelee kuwa himilivu” amesisitiza Waziri Sangu.

‎Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Renata Rugarabamu amemweleza Waziri kuwa mfuko huo ni himilivu na kwamba unaendelea kutoa huduma zake kwa wafanyakazi kwa weledi na ubora.

‎Rugarabamu ameongeza kusema Mfuko wa WCF utaendelea kuhakikisha wafanyakazi waliopata majanga inawapa fidia ili waweze kurudi katika jamii kuendelea kutoa mchango wao kwenye ukuaji wa uchumi ambapo alibainisha kuwa mfuko umeongezeka toka shilingi Bilioni 26 mwaka 2024 hadi shilingi Bilioni 51 mwaka 2025 hatua inayoufanya uwe  himilivu.

‎Waziri Sangu amekutana na Bodi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Waziri mwenye dhamana ya sekta ya kinga ya jamii ambapo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni moja wapo. Taasisi zingine zinazotekeleza kinga ya jamii ni Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!