Latest Posts

SERIKALI KUNUSURU UPOTEVU WA MACHUNGWA TANGA

Serikali imeandaa mkakati kabambe wa kunusuru upotevu mkubwa wa zao la machungwa mkoani Tanga kwa kuandaa kongamano maalum litakalowaleta pamoja wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuwekeza kwenye mnyororo mzima wa zao hilo.

Hayo yamebainishwa Jumanne Julai 15,2025 katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk. Batilda Burian, wakati akieeleza  mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema   kongamano hilo linaandaliwa kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Kongamano hili litaanza kwa kuangazia kwa kina zao la chungwa kwa msimu huu, machungwa yamekuwa mengi sana sokoni na bei imeshuka mno, hali ambayo imesababisha upotevu mkubwa. Tumeona tuanze na hili ili kuvutia wawekezaji makini watakaosaidia kuongeza thamani ya zao hili,” amesema Dkt. Burian.

Amebainisha kuwa kwa sasa kuna kiwanda kidogo cha kusindika maganda ya machungwa mkoani humo, lakini kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa wawekezaji na rasilimali.

“Tunalenga kuendeleza mnyororo mzima wa zao la chungwa – kuanzia maganda, juisi, hadi bidhaa nyinginezo. Kwa kifupi, machungwa ni utamu mwanzo hadi mwisho. Tunaamini kufikia mwisho wa mwaka huu tutakuwa tunazungumzia mafanikio mapya,” Ameongeza .

Kuhusu ukusanyaji wa mapato, Dkt. Burian amesema  Mkoa wa Tanga ulipangiwa kukusanya Shilingi bilioni 47.2 kwa mwaka wa fedha uliopita, ambapo umefanikiwa kukusanya Shilingi bilioni 44.68 – sawa na asilimia 95 ya lengo.

“Upungufu wa asilimia tano umetokana na changamoto za makusanyo katika baadhi ya viwanda, hususan vya saruji, kutokana na utata kuhusu tozo za kodi. Suala hili kwa sasa liko kwenye mchakato wa usuluhishi,” ameeleza .

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!