Latest Posts

SERIKALI YAKWAA KISIKI TUME YA KUCHUNGUZA MATUKIO YA OKT. 29/ UCHUNGUZI KUENDELEA

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imewaruhusu waleta maombi kufungua kesi ya msingi, katika shauri namba 30210/2025 linalohusu kupinga uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua Tume Huru ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani nchini yaliyotokea Oktoba 29 mwaka huu na siku zilizofuata
Hata hivyo, licha ya Mahakama kuruhusu waleta maombi kufungua kesi msingi ndani ya siku 14 kuanzia leo, lakini imekataa ombi la kuzuia kwa muda shughuli za Tume hiyo hadi pale kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi
Katika uamuzi wake uliosomwa leo, Alhamisi Desemba 18.2025 na Naibu Msajili wa Mahakama Hussein Mushi kwa niaba ya Jaji Hussein Salum Mtembwa aliyekuwa anasikiliza maombi hayo, Mahakama imesema imesema kila upande utabeba gharama zake
Katika shauri hilo lililoendeshwa leo kwa njia ya mtandao, upande wa Jamhuri ukihuhusisha wajibu maombi wa kwanza ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Wajumbe wote Nane wa Tume hiyo wakiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman ulikuwa unakilishwa na Wakili wa Serikali Waandamizi Daniel Nyakia na Wakili wa Serikali Erigh Rumisha, mjibu maombi wa 10 ambaye ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimewakilishwa na Wakili Ferdinand Makore, wakati waleta maombi ambao ni Rosemary Mwakitwange, Edward Heche na Deogratias Mahinyila wamewakilishwa na Wakili Hekima Mwasipu
Akizungumza na Jambo TV, muda mfupi baada ya uamuzi huo Wakili Hekima Mwasipu amesema kwa niaba ya wateja wao wamepokea uamuzi huo kwa moyo mkunjufu, na kwamba watatekeleza maagizo ya Mahakama ndani ya muda waliopewa
Hata hivyo, Wakili Mwasipu amesema watafungua kesi hiyo kwa hati ya dharura, na kwamba watawasilisha tena maombi Mahakamani hapo kuomba Tume hiyo izuiliwe kwa muda kufanya kazi hadi hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi
Akizungumza kwa niaba ya TLS, Wakili Ferdinand Makore amesema wao wamepokea uamuzi huo kwa mikono miwili, na kwamba katika maombi hayo wamehakikisha wanasimama upande wa waleta maombi, lakini pia amesema haoni tatizo lolote litakalosababisha kesi hiyo ‘ivurugike’ licha ya kwamba Tume husika inaendelea na kazi.
Tazama video nzima hapa 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!