Latest Posts

SHAHIDI ASKARI ALIVYOVUTANA NA LISSU ‘KWA NINI WAWAACHIE WALIOTAKA KUVURUGA UCHAGUZI’

Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu leo Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kesi ya Uhaini inayomkabili alimhoji shahidi wa 15 Detective Koplo Amani(35) juu ya kumkamata shahidi P3 na kumuachia haliyakuwa shahidi huyo aliieleza mahakama kuwa alikuwa anahamasisha vijana kufanya uasi na kuvuruga uchaguzi kwa kupiga watu mawe.

Shahdi anasema yeye ni Askari Polisi tangu 2012, akifafanyia  kazi Mbeya, wilaya Mbeya Mjini kituo cha Polisi cha kati Mbeya tangu 2012 ambapo ilikuwa tu baada ya kuhitimu mafunzo alipangiwa Mbeya.

Anaeleza pale kituoni yupo kitengo cha upelelezi makosa ya kijinai akiwa chini ya Ofisi ya Mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Mbeya OCCID ambapo yeye ni kama msaidizi wa shughuli zote za upelelezi ndani ya Wilaya ya Mbeya mjini.

Anaeleza majukumu yake ni kufanya doria, kufanya upelelezi, kukamata watuhumiwa wa makosa ya jinai na kuhakikisha wanafikishwa mahakamani.

Aprili 4, 2025 anasema alikuwa Kituo cha Polisi Ilomba Mbeya alipewa maelekezo na Inspekta Joram Kaimu Mkuu wa upelelezi wilaya ya Mbeya mjini maelekezo ya kwamba aende maeneo ya Isyesye mtaa wa Mwantegule ambapo alimueleza kwamba kuna watu wanapanga kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu 2025.

Anaeleza kuwa aliwasiliana na Askari mwenzanke ambaye yuko kitengo cha Intelijensia ili aende akamuoneshe watu hao wanaojipanga kufanya fujo na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.

Alifafanua kua Askari wa Intelijensia “Ni askari wanaofanya kazi kwa kujichanganya na wananchi kwa ajili ya kupata taarifa muhimu mbalimbali zinazohusiana na uhallifu na uvunjifu wa amani na makosa ya jinai Wengine bodaboda wengine wafanyabishara.”

Baada ya kupata maagizo na kupata namba ya simu aliwasilliana na yule askari mwenzake na kukutana nae maeneo ya Isyesye mtaa wa Mwantegule. Kwa kuwa alishaongea na Inspekta Joram moja moja alimuongoza na kumuonyesha moja kwa moja mtuhumiwa ambaye alipaswa kumkamata (alikuwa kwenye kijiwe cha boda boda akiwa na wenzake).

Taarifa zilikuwa ni kwamba mtu yule ndio alikuwa anahamasisha wenzake kufanya fujo kuharibu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Baada ya kuonyeshwa mtu yule alimfuata akamuita na kumtoa eneo lile la kijiweni na wakakaa pembeni kidogo kisha alijitambulisha kwake kisha akamueleza tuhuma zake za kuhamasisha kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu 2025 unaohusu Rais, Wabunge na Madiwani.

Baada ya kumueleza tuhuma zake akamwambia anahitajika Kituo cha Polisi Ilomba baada ya kumueleza hivyo hakubisha walienda Ilomba. Anasema “Nilipofika pale nilimjulisha Inspekta Joram ambaye alinipa kazi hiyo kisha aknipa maelekezo ya kumuandika accuse maelezo jina lake ni P3 kuhusiana na tuhuma ya kufanya uchochezi na kufanya vurugu kuharibu uchaguzi mkuu 2025. Baada ya hapo nilimuandika maelezo kama nilivyoelekezwa kama mtuhumiwa.”

Shahidi anasema P3 “Alisema ni kweli alikuwa anahamasisha wenzake kufanya fujo kuharibu uchaguzi mkuu 2025 alkuwa akipitia taarifa mbalimbali kwenye mtandao wa YouTube alimsikia mtu ambaye alimtaja Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu akiongea na kutoa kauli za kuhamasisha uasi, kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.”

Anaeleza kuwa alipomaliza alimjulisha Joram akampa maelekezo, mtuhumiwa adhaminiwe na awe anaripoti polisi Ilomba kila baada ya siku tatu.

Aprili 17 2025 akiwq Ilomba alipewa maelekezo Inspekta Joram ya kumuandika mtuhumiwa yule maelezo kama shahidi kuhusiana na kile alichoeleza kwenye maelezo yake kwamba aliona Mwenyekiti wake akihamasisha vurugu kuharibu uchaguzi mkuu aliona kauli ile yeye kama mfuasi wa CHADEMA alihamasika kutokana na kauli zile na alikuwa tayari kuwashawishi vijana mwenzake kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha kufanya vurugu na kuharibu uchaguzi mkuu wa 2025.

Baada ya hapa shahidi akawa amemaliza kitoa ushahidi wake akiongozwa na sasa ukawa wasaa wa Lissu kuuliza maswali ya dodoso.

Lissu: Umesema wewe ni msaidizi wa shughuli zote za upelelezi ndani ya wilaya ya Mbeya mjini kweli si kweli

Shahidi: Sahihi kabisa

Lissu: Waeleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye kielelezo D14

Shahidi: Waheshimiwa Majaji haya maneno Hayapo

Lissu: Umesema kwamba ni askari wanaojichanganya na raia wengine ni bodaboda na Mama Ntilie wanaojichanganya ili wapate taarifa mbalimbali

Shahidi: Ni sahihi kabisa

Lissu: Umesema baada ya kupewa namba ya mtu wa Intelijensia uliwasiliana nae na baadae ukakutana nae Isyesye. Waeleze majaji kama hayo maneno yapo kwenye kielelezo

Shahidi: Hayapo

Lissu: Umesema kwamba huyo askari wa Intelijensia alikuongoza na kukuonyesha mtuhumiwa uliekuwa unapaswa kumkamata. Waeleze majaji kama ushahidi huo upo kwenye kielelezo D14

Shahidi: Haupo kwenye kielelezo

Lissu: Umesema kwamba tuhuma iliyokuwa inamkabili ni kinyume cha kifungu cha 390 cha kanuni ya adhabu

Shahidi: Kweli

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama katika maelezo yako tuhuma iliyokuwa inamkabili ni kufanya makosa kinyume na kifunhu cha 390 cha Kanuni ya adhabu

Shahidi: Hayapo

Lissu: Shahidi umesema baada ya kuandika maelezo ya mtuhumiwa ulimjumuisha Inspekta Joram Acting OCCID akakuelekeza kumuachia mtuhumiwa kea dhamana awe anaripoti kila baada ya siku tano kwa dhamana. waeleze Waheshimiwa Majaji kama hayo maneno yapo kwenye kilelele D14.

Shahidi: Yapo

Lissu: Yako wapi

Shahidi:

Lissu: Wapi ambapo Inspekta Joram alikuelekeza kumuachia kwa dhamana

Shahidi: Hayo sikuandika

Lissu: Ushahidi tarehe 17.4.2025 wakati nikiwia kituo cha polisi Ilomba niliekeleza na Inspekta Joram kuandika meelezo ya mtuhumiwa kama shahidi kuhusiana na kile alichoeleza mtumhmiwa juu ya Mwenyekiti wake Lissu akahamasika nas kuhamasisha vijana wenzake kufanya vurugu juu ya uchaguzi Mkuu wa 2025. Waelze majaji kama hayo maneno yapo kwenye kielelezo D14

Shahidi: hayapo

Lissu: Maelezo uliyoyasema hapa ni muhimu ndio maana na hukuandika kwenye kielelezo D14

Shahidi: Kweli

Lissu: Waeleze majaji kama maelezo hayo ni muhimu na sababu ya kutoyaandika.

Shahidi: Sijayasema kwa sababu mahakama bado inaendelea

Lissu: Ulisema kwamba askari wanaojichanganya na raia ili wapate taarifa na P3 ni dereva bodaboda

Shahidi: Kweli

Lissu: Kwa hiyo ni kweli au si kweli kwamba P3 ni Polisi wa Intelijensia wa kwenu

Shahidi: Sio Kweli

Lissu: Waeleze majaji huyu P3 alikua anahamasihaa vijana kufanya vurugu kwa maelezo yako unasema alikuwa anapanga kupiga watu mawe anafanya uasi, kufanya vurugu kupiga watu mawe halafu ulivyomuhoji boss wako akakuambia umpe dhamana. Mti anaetaka kufanya uasi ukampa dhamana. Hii inaingia akilini

Shahidi: Inaingia

Lissu: Kama hii inaingia ni ajabu kwamba Oktoba 29 ilileta maafa kwa sababu kuna watu walipanga maafa mkawaachia. Mkampa dhamana mtu anaetaka kufanya uasi mkamwambia kazi yakocni kuripoti kila baada ya siku tatu

Shahidi: Kweli

Lissu: Waeleze Majaji kama mlimpeleka Mahakamani kwa kufanya uasi

Shahidi: Hayo majibu sina mimi

Lissu: Ulipoulizwa majukumu yako ulisema ni  kufanya dorua kupeleka kesi kufanya doria na kufikisha mahakamani wote tuliowakamata kwa makosa ya jinai. Kweli si kweli

Shahidi: Kweli

Lissu: Umesema P3 alikua bodaboda

Shahidi: Kweli

Lissu: Waeleze majaji kama kwemye maelezo umeweka maelezo kama alikua na aina gani ya pikipiki

Shahidi: Hayapo

Lissu: Ulileta namba ya pikipiki

Shahidi: Plate za pikipiki inahusianaje na kesi hii

Lissu: Inaonyesha ni bodaboda

Shahidi: Kwa hiyo akisema mkulima tulete shamba

Lissu: Sasa wewe unanihoji mimi

Shahidi:

Lissu: Huyu mtuhumiwa ulipomfikisha Ilomba ulimuweka mahabusu kweli si kweli

Shahidi: Si kweli

Lissu: (anasoma kielelezo D12) maelezo ya P3 juu ya kilichotokea alipopelekwa Ilomba alisema “tulipofika kituoni aliniweka mahabusu baada ya muda kidogo nilitolewa naxkwenda kuhojiwa”. Swali langu kati ya ushahidi wako wewe kwamba hukumuweka mahbusu na P3 kwamba ulimuweka mahabusu Mahakama ichukue ushahidi upi.

Shahidi: Mahakama itaamua

Lissu: Umesema kwamba P3 alikua anahamasisha watu kupigwa mawe

Shahidi: Ni sahihi

Lissu: Swali langu mbona hiyo hukuisema hapa mahakamani.

Shahidi: Nimeshaeleza si kila kitu cha kusema. Nashukuru Mungu kwamba unalifahamu

Lissu: Ni kweli si kweli kwamba P3 alikuambia yeye ni mwanachama wa CHADEMA

Shahidi: Sio kweli

Lissu: Wewe ndio uliyeandika maelezo yake kweli si kweli

Shahidi: Kweli

Lissu: Ngoja nikusomee ulichoandika ‘mimi pia ni mwanachama/mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa hiyo alikuambia ni mwanachama na mfuasi wa CHADEMA, Kweli si kweli

Shahidi: Kweli.

Lissu: Alikuonyesha kadi yake ya uanachama

Shahidi: Sikumuuliza

Lissu: Alikuambia wafuasi wa CHADEMA wanatambulikaje

Shahidi: Sikumuuliza

Lissu: Waeleze majaji kama ulimrekodi kwenye daftari la mahabusu

Shahidi: Mimi nimesema sikumuweka mahabusu

Lissu: Ni kweli au si kweli Polisi inapotokea taarifa ya aina hiyo wanafungua Jalada la Uchunguzi

Shahidi: Ni sahihi

Lissu: Waeleze majaji baada ya maafa yote ya Oktoba 29 kama mmemchukulia hatua yoyote huyu aliyesema anatakupoga watu mawe

Shahidi: Sifahamu

Lissu: Mashahidi wa kificho ambao wamekuja kutoa ushahidi hapa mahakamani ni bodaboda au machinga unafahamu.

Shahidi: Sifahamu

Lissu: Ulichukua hatua gani kuhakikisha kama haendelei na uhamasishaji wa uasi

Shahidi: Sikupewa hiyo kazi

Lissu akawa amemaliza kuuliza maswali yake ya dodoso ambapo mahakama ilitoa nafasi kwa upande wa mashtaka kuuliza maswali ya kusawazisha maswali ya dodoso.

Mahakama iliahirisha shauri hili mpaka Jumatatu Februari 23 ambapo litaendelea saa tatu asubuhi

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!