Na Theophilida Felician, Kagera.
Wanachama cha waganga nchini TAMESOT mkoa Kagera wamesikitishwa na kifo cha mwaasisi wao marehemu Sadiki Nuru Hassani kilichotokea ghafla manispaa ya Bukoba.
Baadhi ya viongozi wa chama hicho wameungana na dugu na wananchi kwa ujumla kumuombea dua marehemu Sadiki Nuru ambaye alikuwa nguzo muhimu kwa chama na tiba asili ambapo katibu wa chama mkoa Bw Patiani Kashubi kwaniaba ya viongozi wenzake baada ya kukabidhi rambirambi ya chama taifa na mkoa kwa familia amesema marehemu aliishi na kufanya kazi ya tiba asili kwa ushirikiano mkubwa, alitoa ushauri, alipenda umoja mshikamano kwa waganga wenzake, alikuwa ni mtu wa kumcha mwenyezi Mungu jambo lililomwezesha kufanikiwa vyema katika utendaji kazi wake wakuwahudumia tiba wananchi.
Katibu Patiani amewasihi waganga wa tiba asili kuyaishi nakuyaiga mema yaliyotendwa na marehemu huyo enzi za uhai wake huku akitoa wito kuendelea kufanya kazi kwakuzingatia misingi na miongozo ya sekta hiyo kama yalivyo maelekezo ya serikali kwa lengo la kuziepuka changamoto wanazoweza kukabaliana nazo.
Alliy Nuru Hassani ni mdogo wa marehemu amesema kuwa Sadiki aliugua ghafla zikafanyika juhudi na kumpeleka hospitali ya Zamzam ambapo muda mfupi alikata roho wakati madaktari wakihangaika kufahamu ni ugonjwa gani uliomsumbua.
Amewashukuru TAMESOT kwa namna walivyokuwa nao kama familia tangu mazishi hadi kumuombea dua huku akiwaomba wazidi kuwa na utaratibu huo wakusaidiana kama wanachama kwenye shida na raha.
Viongozi walioshiriki dua hiyo iliyofanyika nyumbani kwao mtaa wa Buyekela kata Bakoba nakuongozwa na shekhe wa wilaya Yusuphu Kakwekwe ni pamoja naye mwenyekiti wa TAMESOT mkoa Halima Rwiza, Ally Mohamed Ally mwenyekiti manispaa ya Bukoba na Ramadhani Rashidi Katibu wilaya Misenyi na wanachama wengine kwa pamoja wameeleza kuwa kifo cha Sadiki Nuru ni pengo kubwa kwa tiba asili Kagera na taifa.