Latest Posts

TRIL . 1.56 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA

Katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Mkoa wa Shinyanga umepokea zaidi ya shilingi trilioni 1.563 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyaga Mbona Mhita, ameeleza mafanikio haya kama kielelezo cha dhamira ya Serikali kuboresha ustawi wa wananchi, hasa katika upatikanaji wa huduma za maji safi, afya, elimu na usafiri.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 14,2025 jijini Dodoma, wakati akieeleza Mafanikio ya  Serikali ya Awamu ya Sita Mhita amesema pia kuwa mkoa umeongeza ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 98, huku miradi mingi ikitekelezwa kupitia fedha hizo. Mafanikio haya yamechangiwa na ushirikiano wa wananchi, elimu ya mapato, na uwekezaji katika sekta ya madini.

Aidha, amesema Mkoa umepokea kiasi cha shilingi bilioni 113.33 katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 kwa ajili ya huduma ya maji , “Mafanikio makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na Kuimarika kwa huduma ya upatikanaji wa maji safi kwa wananchi wa Mkoa kutoka asilimia 63 mwaka 2020 hadi asilimia 79, mwaka 2025 maeneo ya mijini na asilimia 51 mwaka 2020 hadi asilimia 68 mwaka 2025 vijijini”.

Amesema Kuongezeka kwa idadi ya vijiji 222 vyenye huduma ya maji kutoka Vijiji 162 mwaka 2020 hadi Vijiji 384 mwaka 2025, Kukamilika kwa miradi 64 na kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini na kuendelea na utekelezaji wa miradi 75 iliyofikia wastani wa asilimia 62; Kuendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria katika Vijiji 111 katika maeneo ya Kishapu, Shinyanga na Kahama.”

Mhita ameendelea kusisitiza Mkoa umepokea shilingi bilioni 79.1 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya.

“Kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2020/21 hadi Machi, 2025, Mkoa wa Shinyanga uliidhinishiwa kukusanya mapato ya ndani ya jumla ya Shilingi bilioni 151.87 kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hadi kufikia Machi, 2025, jumla ya Shilingi bilioni 150.26 zilikusanywa, sawa na asilimia 98,”

“Fedha hizi zilikusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama Fedha za Uwajibikaji wa Taasisi kwa Jamii yani CSR (Hatukuishia kwenye local content), ushuru wa mazao na mifugo, pamoja na ada mbalimbali zinazotozwa na halmashauri mfano ada za leseni za biashara na mirabaha katika sekta ya madini. Katika fedha hizo miradi yenye thamani ya Tsh. bilioni 65.5 ilitekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na ukamilishaji wa maboma ya katika sekta za elimu na afya, ikiwemo Ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wazazi na Watoto Hospitali ya Manispaa Kahama lenye thamani ya shilingi bilioni 6.8”, ameeleza na kuongeza,

“Katika kipindi cha miaka minne (Machi 2021 hadi Aprili 2025), Mikoa ya Kimadini ya Shinyanga na Kahama imekusanya mapato ya jumla ya Shilingi bilioni 540.17. Aidha, kwa mwaka 2024/2025 hadi kufikia Aprili 2025 kiasi cha Shilingi bilioni 131.51 kimekusanywa ikilinganishwa na lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 165 sawa na asilimia 79.70. (Elimu)”.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!