Latest Posts

TUNA MUDA MIEZI MITATU YA KUKAA MEZANI NA KUONDOA DOSARI ZA UCHAGUZI- DKT. KITIMA

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, amewashauri viongozi wa kisiasa nchini, serikali na wadau wote wa uchaguzi kukaa mezani haraka iwezekanavyo ili kujadiliana na kuondoa dosari zilizozua sintofahamu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Jambo TV, Padri Kitima amesema bado kuna muda wa kutosha kwa pande husika kuzungumza kwa nia njema ili kuhakikisha Watanzania wanashiriki uchaguzi huru, wa haki na wenye kuaminika.

“Watu wakae mezani, yanayoweza kufanyika sasa yafanyike. Hii ni Julai, bado kuna Agosti na Septemba. Muda haujaisha. Dosari hizi zimewakera wengi, tuziondoe,” amesema Padri Kitima.

Ameeleza kuwa, badala ya kutaka kususia uchaguzi, viongozi wa vyama vya siasa waamini kuwa serikali inaweza kutoa ahadi ya kweli na yenye dhamira ya kuondoa vitendo vya udhalimu na kutozingatia sheria katika mchakato wa uchaguzi.

“Wanaotaka kususia uchaguzi waamini kwamba ahadi itakayotolewa na serikali kwamba hizi dosari hazitakuwepo, waamini kweli dosari hizo hazitakuwepo, na wakishaamini washiriki, halafu siku ya uchaguzi watakapoona zimekiukwa basi watakuwa na fursa ya kuthibitisha kwamba basi kwa mantiki hii labda twende mahakamani, au kwa mantiki hii hayo mabadiliko yafanye kwa lazima kupitia serikali mpya itakayokuwa imeingia, lakini kusema kwamba lazima tukae tubadilishe sheria zote na nini ndani ya muda uliobaki au tuahirishe uchaguzi binafsi ninaona kule tunaenda mbali mno, hebu turudishe kwanza uadilifu, na kuondoa dosari hizi”, ameeleza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!