Latest Posts

TUVUNJE MAKUNDI YETU TUPAMBANIE USHINDI-KOOLA

Mgombea Ubunge Jimbo la Vunjo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Enock Koola amesema kuwa wakati wa makundi umefika mwisho na sasa ni wakati wa kupambania ushindi.

Ametoa kauli hiyo Agosti 26,2025 wakati akichukua fomu ya uteuzi katika ofisi za tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Halmashauri ya Moshi.

Akizungumza kuhusu mwenendo wa uchukuaji fomu za uteuzi, Msimamizi wa uchaguzi Majimbo ya Moshi Vijijini na Vunjo Lucas Msele amesema kuanzia Agosti 14 hadi Agosti 26 majira ya saa nane mchana jumla ya vyama 19 vimechukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika majimbo hayo ambapo vyama 9 ni Jimbo la Moshi vijijini na 10 Jimbo la Vunjo.

“Kwa Jimbo la Moshi Vijijini vyama vilivyochukua fomu mpaka sasa ni pamoja na CUF,CCK, ADATADEA,TLP, CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI,ACT WAZALENDO,CHAUMMA na CCM huku Jimbo la Vunjo ikiwa ni DP,ACT WAZALENDO,ADATADEA,CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI,CCK,AFP,TLP, CHAUMMA,NRA na CCM” alisema Msele.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!