Latest Posts

VIKUNDI VINAVYOPATIWA MIKOPO GEITA VYATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA

Vikundi vinavyopatiwa mikopo ya asilimia 10 kutoka kwenye mapato ya ndani ya halmashauri vimetakiwa kuhakikisha vinatumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili ziweze kuwanufaisha kiuchumi badala ya kuzitumia kwenye matumizi yasiyo na tija.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, wakati wa zoezi la ugawaji wa mikopo kwa vikundi 100 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Geita, yenye thamani ya shilingi bilioni 1.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Geita, Costantine Morandi, amesema halmashauri hiyo imepiga hatua kubwa katika utoaji wa mikopo hiyo, ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo, akiwemo Frank Bukela na Lucia Khalfan, wameeleza furaha yao na kutoa shukrani kwa serikali, hususan Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa mikopo hiyo kwa wananchi.

Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri inalenga kujenga jamii inayojitegemea kwa kujiajiri na kubuni vyanzo endelevu vya mapato, hivyo kusaidia katika kuinua maisha ya wananchi kiuchumi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!