Latest Posts

VIONGOZI WANAWAKE WATAKIWA KUTOJIBWETEKA NA VYEO, WAJENGE UWEZO WA KUJIFUNZA DAIMA

Katibu Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Zena Ahmed Said, amewataka viongozi wanawake 70 wanaoshiriki mafunzo ya wiki moja ya uongozi kutoka taasisi mbalimbali, kutojibweteka kwa majina au vyeo walivyonavyo, badala yake wawe na moyo wa kujiendeleza kila mara na kubadilishana uzoefu na watendaji wenzao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, yanayofanyika kwa mara ya tatu katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha, Zena amesema watoto wa kike wanapaswa kujiamini katika nafasi mbalimbali wanazopata, kuanzia kwenye familia zao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Uongozi, Profesa Marcelina Chijoriga, amesema mafunzo hayo yanashirikisha washiriki kutoka taasisi 19 za serikali, huku washiriki wengine wanne wakijilipia wenyewe kutokana na utashi wa kujiendeleza binafsi.

Baadhi ya washiriki wamesema wana imani kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo katika kazi zao pamoja na kuongeza mshikamano na ushirikiano na wenzao.

Mhandisi Anifa Chingumbe, Kaimu Meneja wa TTCL Mkoa wa Kagera, ameishukuru Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere kwa mafunzo ya awali aliyopata, akieleza kuwa yamemsaidia kupanda cheo.

Naye Julieth Lyimo, Kiongozi wa Mtandao wa Wanawake Mkoa, amesema Shule hiyo haitoi mafunzo kwa vyama na makada wa siasa pekee, bali pia kwa taasisi binafsi na watu mmoja mmoja wanaokidhi vigezo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!